Dondoo 10 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote


🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
🌿Mkanye mtoto wako wa kike na hata wa kiume kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.
🌿Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.
🌿Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu”.
🌿Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi....
🌿Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda kwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.
🌿Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.
🌿Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za siri mwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.
🌿Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.
🌿Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.
🌿Usipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!!
*_Kama unadhani Dondoo hizi ni Muhimu.Tafadhali soma na uwapelekee wengine_*
May be an image of one or more people and text

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA