FAHAMU KIASI CHAMAJI UNACHOPASWA KUNYWA KULINGANA NA UZITO WAKO
Ni kiasi gani cha maji unakunywa kwa siku na unakunywa wakati gan!
Kama tunavyojua kuwa maji ni uhai, maji yakinywewa kwa nidhamu na kuzingatia uzito mtu alionao tunaweza kukwepa zaidi ya asilimia sitini (60%) ya maradhi mbalimbali.
Muda gani sahihi wa kunywa maji!
Mara tu unapoamka asubuhi.
Nusu saa au dk 45 kabla ya muda wa chakula cha mchana au cha jioni.
Na muda uliobaki kunywa kiasi kwa kipindi fulani cha muda.
Yanywe maji ukiwa umekaa na kunywa kidogo kidogo.
Muda gani usinywe maji!
Usinywe maji wakati au mara tu baada ya kula. Ijulikane kuwa maji na chakula ni vitu viwili tofauti ambavyo mwili unahitaji lakini sio kwa mkupuo. Ukifanya hivyo maji yanaharibu baadhi ya virutubisho vilivyopo kwenye chakula.
Usinywe maji mengi kwa wakati mmoja ili kufikia kiwango kinachohitajika kwa siku.
Hakikisha inapofika saa 12 jioni uwe umeshafikia kiwango chako cha mwisho, usinywe maji zaidi ya muda huo yatakuharibia usingizi usiku.
Kiasi gani cha maji ninywe kwa siku kulingana na uzito nilionao!
Angalia kwenye picha iliyoambatanishwa chini ya makala hii upate kujua kiasi unachotakiwa kunywa kulingana na uzito ulionao.