JIFUNZE NAMNA YA KUMSAHAU ALIYE KUUMIZA KWENYE MAPENZI


Wengi mioyo yetu imejaa maumivu baada ya kutendwa na watu tulio wa penda na kutaman kudum nao.Tumejikuta ktk wakat mgum sana na mda mwingine kuhis hatuwez Fanya lolote bila wao.
Fanya haya kumsahau
1. Acha kumuongelea
Usipende kumuongolea kwa watu mtu ambae mumeachana au unataka kuachana nae sababu ya usalit. Utapo kuwa una muongelea utaendelea kumkumbuka... Wapo ndugu au rafik watakao uliza habar zake,usiwape ushirikiano mzur na waoneshe hutak muongelea
2. Usiwasiliane nae
Mawasiliano hufanya watu kuwa karibu. Hivyo acha kutuma wala kujibu SMS au simu za MTU ambae hutak aendelee kuumiza moyo wako. Kuendelea kuwasiliana nae utaishia kujitesa,hasa ikitokea yeye bado anakujibu vibaya
3. Kumbuka mabaya yake
Kwa kipind chote ulicho kuwa nae jaribu kuku kumbuka mambo aliyp yafanya yakaumiza moyo wako. Ukikumbuka mazur utaishia kuumia na kutaman kurudiana nae
4. Tumia vizur mda wako
Kama we mfanya kaz,mfanya biashara au mwanafunz,bas kuwa bize na kile unacho kifanyaa. Ukiwa bize hutopata mda wa kumfikiria,mwil na akil vikichoka utajitupa tu kitandan na kulala
5. Tafuta marafik kubadilishana mawazo.
Ili kuepuka kuwa mpweke tumia mda wako mwingi kutafuta marafik wapya. Kuptia wao kuna meng utajifunza na kupata ujasir upya kuukabili upweke
6. Anzisha uhusiano mpya.
Kikawaida unapo ishi bila mpenz ni rahis kuendelea kumkumbuka wa nyuma. Ni mwaka au zaid yangu uachane nae,afu bado unaogopa kupenda au kupendwa tena..
Dawa ya penz ni penz,ili uweze msahau mtu wako lazima umpate mtu ambae atakuwa angalau na mazur ya kukufanya ufurah. . huwez msahau kwa kuendelea kuwa SINGLE..... Usiogope kupenda kwa kuhofia kuumizwa,ni maisha tu
7. Safiri
Kuna mda waweza jipa rikizo ukaenda sehem kutuliza akili yako kwa siku hata 2. Waweza tembelea ndugu au rafik zako popote iwe nje au ndan ya mkoa wako.... Kusafir kutakufanya urud na akil mpya.
8. Jiamini na jikubali
Usijione munyonge na una mapungufu kisa yeye amekuacha au kukusaliti. Kama yeye aliweza kubali kuwa nawe bas yupo mwingine utampata. Bado we ni bora na unazo sifa zote.. Jiamini kuwa utampata mtu bora zaid yake
9.Usifuatilie maisha yake
Acha kumfuatilia X wako eti ujue saiz yupo wap ana ana mahusiano na nani. Mara kufuatilia status zake.kuendelea kumfuatilia ni kujiumiza tu. Mwache aendelee na yake nawe fuata yako.
10. Usimuoneshe huzuni
Ni kosa kubwa sana kumfanya mtu ajue kuwa unaumia kwa ajili yake . yaan ktk mitandao una post maneno yenye kuonesha una umia,unaweka status za nyimbo zenye kuelezea maumivu. Hali hii itakufanya ulie tu huku yeye akifurahia uwepo wake ktk mawazo yako.
Kumbuka
Kama mtu hakutak na ameamua kukutupa hata ujishushe vipi hawez kukuelewa. Hawez kukurudia.
Hata akikurudia ataendelea kuku umiza Mara kwa Mara..
Usimulazimishe akupende kisa unampenda. Usimlilie kisa unampenda..
Mapenz yana raha na furaha
Ukipenda na kupendwa
Ukiheshim na kuheshimiwa
Ukiamin na kuaminiwa
Nje ya hapo utakuwa unajipendekeza na kulia kila siku.
Achana nae
Yupo bora kwa ajili yako
Mungu atakukutanisha nae.
May be an image of 1 person, child, standing and food

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA