Jinsi ya kumshawishi mwanaume akuoe
Kumfanya mwanaume aweze kuwa na majukumu ya kimaisha ni vigumu, lakini hizi mbinu ambazo tuko nazo za kumfanya mwanaume akuoe zitahakikisha umesimama na yeye madhabahuni haraka sana.
Hivi wewe umekuwa katika mahusiano na mwanaume kwa muda mrefu mpaka unaanza kushuku iwapo huyu mwanaume yuko serious na wewe ama anakuchezea tu? Na umekuwa kila siku ukimwomba Mola akusaidie angalau amfanye huyu mwanaume ulie naye atoe ishara za kuwa atakuoa mbeleni.
Well, sote tunajua kuwa ndoto ya kila mwanamke ni kuwa siku moja katika maisha yake atakuja kuolewa kwa harusi…so sisi hapa tunataka kukupa maujanja ya kumfanya huyo mwanaume atake kukuoa haraka sana.
Jinsi ya kumshawishi mwanaume akuoe;
Kuwa girlfriend kamili. Hivi wewe na mwanaume huyu mumekuwa na maisha ya fanaka. Nyote wawili mumeinjoy maisha ya furaha, mumezama katika mapenzi, na unaona kwamba una uwezo wa kumwambia kila kitu ambacho unakifikiria. Lakini hebu ngoja kidogo na ufikirie mambo ambayo unaweza kufanya zaidi ya hayo.
Mfanye ajihisi kuwa anakubalika, yuko salama na special, haya ndio mambo ambayo anahitaji zaidi. Bila shaka utakuwa unamjua zaidi ya mtu yeyote yule. Kile ambacho anapenda na kuchukia, na mambo ambayo yatamfanya akuone kuwa wewe unapendeza zaidi ya kitu chochote kile.
Hakikisha unafanya kila kitu ambacho mwanamke kamili anaweza kufanya. Mwonyeshe kila kitu ambacho anahitaki, na bila shaka atakuona wewe umejitweka jukumu la kuhakikisha kuwa wewe uko hapo kwa ajili yake.
Mtunze. Kama mwanaume anahisi kuwa hawezi kuishi bila wewe, basi bila shaka atahakikisha ametia kufuli jambo hilo.
Hakikisha kuwa unamtunza na unamfanya akutegemee kwa mambo madogo madogo, hata kama ni jambo rahisi lile la kushughulikia nguo zake ama kumpa sapoti wakati anapohitaji. Wewe kuwa ubavuni mwake kutafanya mabadiliko ya haraka sana, na hatoweza kustahimili kuishi bila wewe.
Kuwa shabiki wake mkuu. Jeuka shabiki mkuu wa mwanaume wako. Kitu chochote kile ambacho ayaamua kufanya, hata kama ni jambo la utani ama la kuchekesha wewe mpe sapoti kwa kumshabikia atimize azma yake.
Ile siku ambayo atakuja kugundua kuwa mafanikio yake katika azma yake yamechangiwa na wewe basi atakuweka karibu yake. Atakuona kuwa wewe umekuwa karibu yake bila hata kupoteza imani katika azma yake. Well utakuwa umetoboa.
Kuwa mkweli kwa kile unachotaka. Wanaume wengi si wajuzi wa kusoma akili ya mtu. Wakati mwingine unaweza kuwa katika mahusiano na mwanaume kwa miaka mingi na ukashangaa ni kwa nini mwanaume kama huyu hajakuposa. Kuna uhakika mkuu ni kuwa wazo kama hilo bado halijamlenga kwa kichwa chake.
Kama umekuwa na maongezi ya ukweli na mwanaume wako, na ukaweka wazi kuwa unampenda, na ukaeleza vile ambavyo unaona mahusiano yenu yatakuwa miaka inayokuja, basi anaweza kuingiwa na hali ya kutaka kuchukua hatua ya mbele kuhusiana na unavyosema. Hata kama hana uhakika na ndoa, atleast utakuwa umeliweka wazo hili katika kichwa chake.
Usimuogopeshe. Usimuogopeshe mwanaume ili akupose kwa kuwa hilo si jambo la kufuata. Inakubalika kuongea maswala ya ndoa, na kueleza msimamo wako. Lakini iwapo utakuwa kila wakati unamtia presha, kila wakati unagusia swala la ndoa, ama kuanza kutokwa na machozi kila upitapo mbele ya duka la harusi basi utafanya ile dhana ya kwake kukuoa kufifia haraka sana kwani atakuogopa.