Kuna kutamani na kupenda haya ni mambo mawaili tofauti hasa linapokuja swala la mahusiano.

 





Kupenda ni process ni jambo ambalo halitokei dakika moja kama wengi wanavyodhani, ni hatua kwa hatua ni jambo ambalo ukua ndani yako kadri unavyoendelea kumjua mtu.

Kutamani ni tendo la glafla hutokea hapo hapo, unaweza kumuona msichana au mwanaume gafla ukamtamani kwa namna muonekano wake ulivyo.
Wengi hutamani na kisha hufikiria wamependa na ndio maana ni rahisi kumuacha mtu bila hata kukufanyia kosa au amefanya kosa la nyinyi kuweza kusuruhishana lakini akili inayokusumbua kichwani kwake ni kukuacha, hii ni moja ya sababu inayoonyeha mwanzoni alifikiri amekupenda kumbe alikutamani namna alivyokuona.
Ni vizuri zaidi ukajipa nafasi ya kumchunguza wewe mwenyewe kama unampenda mtu huyu ama laaah!


Kumbuka kuwa watu waliopendana kweli tokea mwanzoni, vikwazo vidogo vidogo haviwezi kuwafanya wao kuvunja mahusiano yao.
Mtu akikutamkia nakupenda usikurupuke kumwambia na kupenda pia mchunguze vizuri na kwamuda mrefu, asije akawa ni Bomu la machozi kazi yake ni kukutoa machozi tu na utuuzima wako, embu jiulize mzazi wako mwenyewe aliekuzaa hata akusemeje ama akufanyie nn, huwezi toa machozi Leo hii mtu mliekutana ukubwani ndio aje kukutoa machozi ni wapi na wapi.
Chukua hatua machozi yako yanagharama kubwa sana hivyo pata muda wa kumchunguza mwenzio yupo kwako kwa malengo gani na ukiamua kumchunguza utamjua tu mapema, kwani njia ya muongo malanyingi huwa ni fupi sana.


DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA