NGUVU KATIKA MAAMUZI (JUU YA MWENZI WA MAISHA)


Kumbuka - Maamuzi unayoyafanya sasa, ndiyo yenye Nguvu ya Kuamua HATIMA ya Maisha yako ya baadaye. Kila UAMUZI unaofanywa ndio wenye NGUVU ya MATOKEO MEMA au MABAYA katika safari yote ya Maisha ya mbeleni.
Pia Maamuzi ya Mtu katika Jambo lolote yanategemea NGUVU inayotawala Moyo wake, Kama ni Roho Mtakatifu (MATOKEO MEMA) kama ni roho ile nyingine (MATOKEO MABAYA). Huwa hakuna kubahatisha Bali ni UCHAGUZI.
Ulimwengu unazidi kufunikwa na Kele za "HAIWEZEKANI - Vijana wa sasa Kuwa Waaminifu Kama akina Yusufu na Mariam", lakini sauti ya Mungu inazidi kusema "INAWEZEKANA". Tatizo kubwa ni NGUVU ya MAAMUZI, inayotawala akili ya mtu.
Swali lililotanda akili za wengi siku hizi ni, "NITAMJUAJE" kuwa huyu ndiye? au Nitajuaje kuwa sio Mdanganyifu au Mharibifu, au Tapeli wa Mapenzi? ... Swali hili linatokana na Kutomfahamu Mungu. Na huo ndio mkakati wa shetani wa kufanya kila njia, kuwatenga na Mungu, anawatia UPOFU, na hatimaye kutawala nia zao.
Ushauri wa Msingi ili Kufanikiwa:
1. Mpatie Mungu nafasi katika moyo wako ili AKUAMULIE au akupatie NGUVU ya Kufanya MAAMUZI Juu ya HATIMA ya Maisha yako. Neno la Mungu linasema;
... "Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake." Mithali 16:9. Mungu atakuongoza kufanya maamuzi na Kupata Kilicho chema.
"... BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo." 1Samweli 16:7. Kumbuka UZURI wa Mtu kwa Mwenzi wa Maisha, sio SURA ya nje Pekee, huwa Unajengwa Kutoka Ndani. Na ni Mungu pekee, anajua TABIA yenye MDUNDO sawa na wako.
... "Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;" Mithali 3:5. Ukitumia akili yako, ni rahisi Kuona Mtu hana Mvuto na hafai kumbe Ungeruhusu Mungu akuongoze ungemuona tofauti.
2. Jiamini kuwa Mungu ni Baba yako, msikilize yeye. Usiwe na haraka ya Kujibu NDIYO au HAPANA, pata muda mzuri wa Kumuuliza Mungu, yeye atakuamulia na Kulithibitisha ... "Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako." Ayubu 22:28.
May be a black-and-white image of 2 people, people standing, indoor and text that says "BIYI ADELEKE PHOTOGRAPHY"

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA