MNAOVUNJA NDOA ZENU MKIJIFNYA WAJUAJI MSIJEKUSEMA SIJAWAAMBIA!



By idd makengo
(1) Acha kushindana na Mama mkwe, kama hakupigi muache aongee, muache achambe, muache akutukane, yaani muache atapike kuanzia chumbani mpaka sebuleni inama deki!

(2) Wala kisirani chake hakikuhusu wewe, wala hakuchukii wewe! Mama mkwe wako analipa kisasi, alishanyanyaswa na mawifi, katukanywa na Mama mkwe wake, akapigwa na mume wake, analipa kisasi cha matusi ya mwaka 70, muache afumumke!

(3) Huyo si mke mwenza, hamgombanii bwana, wala, anajiona kakuzidi kila kitu ila ukweli nikuwa hajakuzidi chochote, labda alichokuzidi ni uzee tu sasa kwanini kushindana naye!

(4) Huyo ni Bibi tu, ananguvu sasa hivi ndoa changa, ukimpuuza baada ya muda atakua Bibi, atakua anakaa kijijini huko mara moja moja mnamletea wajukuu, yaani hata akiishi muda mrefu akawa ni wakuanikwa kwenye jua lakini akishakua na wajukuu wanajitambua mbona atatulia tu!

(5) Umamuambia Mwanaume mara Mama yake mchawi, mama take ana mdomo, mama yake mchafu, mama yake hivi, mama yake vile! Unataka amfasnye nini Mama yake, mapige, mfukuze, ampe talaka Mama yake au amnyime chakula. Nakuuliza wewe unapomuambia Mwanaume Mama matatizo ya Mama yake unategemea nini?

(6) Kua na kifua Mama, ndiyo ndoa, kama Mama mkwe ni kichomi, mtu akuja kukuletea umbea wa Mama mkwe wako, sema maneno haya “Yule ni Mama yangu namheshimu!” Usitie neno, sikiliza umbea wake ili ujipange kama anakuloga ujue chakufanya ila usitukane, usiongee, usifanye choch0te sema “Yule ni Mama yangu namheshimu!”

(7) Wamama wengi wanakua na mawazo yao, upweke wao, visirani vyao, hat a Mama yako angekua anaishi na Mume wako kuna uwezekano angekua na kisirani na Mumeo angemchoka, mchukulia Kama Mama, muone kama Bibi mtarajiwa na kisha mkumbuke Bibi yako, je ana nafasi gani kwako ukilinganisha na Mama yako, tabasamu na furahia ndoa!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA