MAPENZI YA MBALI; HATAKI UENDE KWAKE ANATAKA AJE YEYE KUKUTEMBELEA.
Mwanzo mlikua vizuri wakati anapata kazi au anahamia sehemu mpya ulikua unaenda, mnatoka pamoja na mnawasiliana vizuri. Tena inawezekana hata ulimsaidia kuhamisha vitu na wakati mwingine hata kodi ya kuanzia maisha ulimpa wewe na kumnunulia baadhia ya vitu. Kila ukipata nafasi ulikua unaenda kwake na alikua anapenda uende wewe kuliko yeye kuja kwako. Ni mke wako, mchumba wako, au ni mume wako, mpenzi wako mnapendana na mna mipango mingi.
Lakini ghafla anaanza kubadilika, kwanza ishu ya kuonana inakua mtihani, una muda na wakati mwingine umechukua likizo kabisa, ni weekend au ni karuhusa kamejitokeza. Ila sasa ukimuambia kuwa unataka kwenda kumuona anaanza sababu, mara nitasafiri, mara nitakua bize kazini kuna wageni wanakuja, sijui kuna ukaguzi utfanyika utakua Bored! Haishii hapo, anakuambia kwanini usisubiri mwezi ujaoa nitachukua likizo au nitaomba ruhusa nitakuja huko.
Ndiyo mpenzi wako ambaye alikua anapenda muonane, kila siku anakuambia amekumiss lakini ukimuambia unataka kwenda kwake yaani inakua ngumu sana, wakati mwingine mpaka mnahombana, anakasirika kuwa unalazimishia sana mambo, anajifanya yuko bize sana, anajifanya eti anakuonea huruma kuwa ukienda utaboreka kutokana na ubize wake. Ndugu yangu ukiona dalili hizi, mpo kwenye mapenzi ya mbali basi jua kuwa huyo mpenzi wako kashapata mtu mwingine.
Lakini sio mtu tu, hapana, ni mtu ambaye wapo siriasi, anaweza kuwa amendanagnya kuwa hajaoa au kuolewa, kamuambia kuwa hana mtu kabisa au kamuambia kuwa mume/mke au mpenzi wake wamgombana na wanakaribia kuachana. Huyo uneyemuita mpenzi mume au mke, anafurahia mapenzi na huyo mtu, inawezekana wanaishi pamoja tayari au hawajaanza kuishi pamoja lakini ni ile kutembeleana kilasiku, pika pakua, kuzunguka kila siku pamoja mpaka majirani wanajua kuwa hawa wanaoana kesho.
Hii ni mbaya zaidi kwa mwanamke, ukiona mwanamke wako anakuambia kuwa siatki uje basi jua kuwa ashampenda huyo mwanaume wake mpya na anakaribia kukuacha. Mwanaume anaweza kuwa ni umalaya tu unamsumbua kwakua wanaume wao hawapendi na mioyo.