DADA ZANGU UKIONA MCHEPUKO WA MUMEO UNAKUTAFUTA JUA KUNA HILI
Dada zangu, ukiona mchepuko wa mume wako unakutafuta basi jua kuwa mambo yashaharibika kwake. Narudia, ukiona mchepuko wa mume wako unakutafuta basi jua kuwa mambo huko yashaharibika.
Anakutafuta wewe, ili akutibue, wewe nawe umtibue mume wako muachane yeye apate nafasi ya kurudiana. Kwa maana hiyo kama una akili, mchepuko wa mume wako ukikutafuta, ukaanza kukuambia sijui niko na mume wako, mimi ndiyo napendwa.
Mwingine ukakuambia, mume wako kanizalisha, sijui kanitelekeza. Kama unaakili utamuambia hivii, kwa mnaokula mnisamehe, jibu ni moja t5u “KAJAMBE MBELE!” Kisha unamblock huyu mwanamke, hufungui meseji zake akituma.
Unanyamaza na hata mume wako humuulizi kitu chochote. Hata mume wako akija kukuuliza flani kanitafuta unamuambia kabisa kuwa sitaki kujua unakua na amani unaishi maisha yako.
Hata kama una hasira, una kisirani basi unaenda chooni unalia kinaishia hukohuko. Lakini kama huna akili sasa, utakasirika, utamsikiliza huyo mwanamke, atakuambia kila kitu, mtaongea na kuonge. Utaenda kumuuliza mume wako, utamtibua.
Utatibua ndoa yako, mtanuniana na mume wako, mtafombana na kupigiana kelele, utatishia na kuondoka, labda utaondoka baada ya wiki yatakushinda utakuja kwangu. Ukija kwangu sasa kwanza nitakuambia ununue Kitabu kwanza, kwamaana nitapata elfu kumi yangu kiulaini.
Baada ya hapo utanipigia simu, nitakukumbusha haya niliyoandika leo kisha nitakuambia rudi kwa mume wako acha kumfuatilia. Dada wameshaachana ndiyo maana mchepuko wamekutafuta, kama ni kukasirika ungekasirika wakati wapo pamoja si kuasubiri mpaka waachane ndiyo ukasirike!