SIMULIZI FUPI YA KUSISIMUA
Mwanamke mmoja alikamatwa na kufungwa gerezani baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya mume wake ambaye mwili wake haukuwahi kupatikana.
Baada ya kutumikia miaka takribani kumi (10) gerezani ikaja kubainika yule mwanaume hakufa bali alimtelekeza mkewe na watoto na yeye kwenda kuishi mbali na mchepuko wake.
Ikabidi taratibu za kumtoa gerezani yule mwanamke zifanyike na siku aliyokuwa anatolewa gerezani mume wake alikuwa ni miongoni mwa waliokwenda akiongozana na ndugu zake wengine kwa lengo la kumuangukia mke wake amsamehe kwa kumsababishia matatizo.
Punde yule mwanamke alipotoka getini akiwa amefura na kwa hasira na kukutana uso kwa uso na mumewe alimpokonya mlinzi wa gereza silaha na kummiminia shaba za kutosha mumewe mbele ya ndugu zake na askari wengine asimpe fursa hata ya kufungua mdomo wake mpaka risasi zikaisha.
Akawageukia askari akasema "nirudisheni gerezani nikaendelee kutumikia kifungo changu kwa kosa lile lile la kumuua mume wangu. Nimetumikia miaka 10 gerezani bila hatia yoyote sasa narudi tena kwenda kutumikia maisha yangu yote gerezani kihalali"
Akawageukia na wakwe zake waliokuja na mumewe kwa lengo la kumuomba msamaha akawaambia "chukueni mzoga wenu mkazike mlinifunga bila ya kosa hamkutaka kusikia maelezo wala kilio changu nikaacha wanangu wakiwa bado wadogo nashukuru sasa wamekuwa kidogo wanajielewa sitojali km watanihukumu kwa kumuua baba yao sababu baba huyo huyo nilishamuua miaka mingi iliyopita sasa narudi gerezani nikiwa na furaha na amani moyoni.
Unahisi huyo mwanamke alichukua uamuzi sahihi au ungekuwa ni wewe ungefanyaje?....
Like kisha share