UKWELI KUHUSU WANAWAKE


1. Mwanamke anapokasirika, zaidi ya nusu ya mambo anayoongea anakuwa hajamaanisha.
2. Wakati mgumu kabisa kwa mwanamke ni pale anapokuwa mbali na mwanaume anayempenda kwa dhati au anapogundua kuwa mumewe ana mahusiano na mwanamke mwingine.
3. Mwanamke sio kama 'tangazo la Omo', usipomjali na kumtunza... wengine wataifanya hiyo kazi badala yako.
4. Inamchukua muda mwanamke kumuamini mwanaume, na akikuamini ni ngumu kumbadilisha, lakini ukijichanganya, sahau kabisa kama atakuamini tena.
5. Mwanamke ni shule ambayo huwezi kuhitimu.
6. Cheti unachopewa unapomuoa mwanamke sio "leseni ya udereva" bali ni kama "kibali cha mwanafunzi".
7. Anaweza kuwa mchungu sasa hivi, lakini baadaye akawa malaika mtamu.. Itategemea namna utakavyoongea naye.
8. Ni ngumu mwanamke kusahau vitu, anakumbuka zaidi yale yanayomuumiza zaidi, hivyo epuka kumuumiza.
9. Mwanamke anaweza kuwa msiri sana.. muda mwingi anapokwazwa na jambo anaenda kwa mtu wake wa karibu, analia.
10. Wanawake wote wanapenda kuombwa. Mara nyingi wanaume wanalisahau hili.
11. Wanawake wote wana tabia y kipekee kama chumvi, unaweza usitambue uwepo wake lakini akikosekana vitu vyote vinakosa ladha.
12. Akikupenda kwa dhati kufanya chochote unachotaka afanye madamu kinakufurahisha, hivyo usimlazimishe kukupenda.
13. Mwanamke akikupenda kwa dhati, hata kukuomba pesa ataona aibu, na hasa kama anakupenda hawezi kuvumilia matumizi yako mabovu ya pesa... hayo ni miongoni mwa mambo yanayowafanya wanawake kuwa viumbe maalum kabisa
May be an image of 1 person, standing, jeep, car and road

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA