Ushauri wangu kwa wanawake.


■Mwanamke usichochee ngono kupitia uvaaji wako wa kikahaba.
■Usiwe unakubali kushikwashikwa na wanaume kwa sababu wanakuona kama Kahaba kwa sababu ya uvaaji wa kikahaba.
■Nguo ya ndani ni siri yako, usikubali kila mtu aione na kuijuia kwa sababu ya uvaaji mbaya.
■Kama wewe ni mwanamke uliyeokoka nakuomba usiwe tai unayetembea kama kuku.
Usiwe kondoo uliyevaa mavazi ya mbuzi.
Usiwe kondoo mwenye tabia za mbwa, hata hapo nazungumza kiroho kabisa.
Usiwe mwanadamu mwenye tabia za majini.
■Matiti yako ni kitu cha thamani sana, usiwe unawaonyesha watu mitaani kwa sababu umevaa nusu uchi.
■Mapaja yako sio choo kiasi kwamba kila mtu anaingia chooni na kuona kukoje.
Kwanza hakuna mwanamke asiye na mapaja, hivyo wewe unayeonyesha mapaja yako mitaani kwa kuvaa nusu uchi huna akili.
■Sehemu zako za siri ni za siri, usizifanye kuwa "sehemu za wazi"
Heshimu utu wako na mwogope MUNGU.
Wimbo Ulio Bora 3:5 "Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe."
●Kumbuka kuvaa kwako nusu uchi kunaleta mitazamo hii kwa wanaume wengi wenye akili.
1. Wanaume wengi wanaokuona nusu uchi wanadhani wewe ni Kahaba.
2. Hakuna mwanaume atakuheshimu kwa heshima sahihi kama wewe ni mtu wa kuvaa nusu uchi.
3. Kama hujaolewa ni vigumu sana kupata mchumba mwenye hofu ya MUNGU.
Utaambulia walevi tu na wazinzi watakaokutesa baadae
4. Wanaume wengi watadhani kwamba umetokea familia yenye malezi mabaya hivyo watakuepuka.
5. Watu wengi wakikuona unavaa nusu uchi watakuchukulia kama mwanamke Malaya na mpenda ngono.
6. Wanaume wengi wanapokuona unavaa nusu uchi watadhani kwamba wewe umeshachafuliwa sana kingono na wanaume wengi, au umeshaambukizwa magonjwa ya zinaa hivyo unatafuta wa kumwambukiza, hivyo wao watakuogopa.
Ndugu, nakuomba badilika kuanzia leo.
Vaa nguo za kujisitiri kama inavyowapasa wanawake wacha MUNGU Katika KRISTO YESU Mwokozi.
1 Timotheo 2:9 " Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa MUNGU."
Jitenge mbali na ubaya wa kila namna ikiwemo kuvaa kikahaba mbele za watu.
1 Wathesalonike 5:22 " jitengeni na ubaya wa kila namna."
Kama wewe ni Mteule wa KRISTO unayejiandaa kwa ajili ya uzima wa milele basi mtii KRISTO na Neno lake.
MUNGU akubariki sana kama ukizingatia.
May be an image of 1 person, standing and indoor

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA