USIRUHUSU TABIA HII ITAWALE MAISHA YAKO

Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani ni tabia isiyofaa. Hakuna mwanadamu aliyeumbwa ili ashindwe,, sote tu washindi zaidi, tunatofautiana njia za kufikia huo ushindi.

Rafiki yawezekana umeshajidharau na kujitamkia maneno kadha wa kadha ambayo kimsingi yamekukatisha tamaa kabisa ya kufikia lengo fulani maishani na ukabaki kushuhudia mafanikio ya wengine kila siku maishani.

Embu ondoa dhana ya kushindwa na kujidharau katika kila hatua upitiayo maishani haijalishi umeshindwa mara ngapi, jifunze kuwa na moyo mgumu na wa subila kwa kila hatua upitiayo maishani,, haijalishi upo katika hali gani? Maishani.

Kama ni maskini sana, usijidharau na umaskini wako ukaona wewe ni wa hali hiyo hiyo maisha yako yote,, hapana, haukuumbwa ili uje kuwa maskini. Ila ni juhudi zako mwenyewe ndizo zitakazokutoa katika umaskini ulionao, haijalishi wewe una ulemavu wa aina yeyote ukajidharau na kujiona huwezi fanya lolote mbele ya jamii likakubalika.

Rafiki kuna walemavu kama wewe, wamejitambua na wameamu, hakika wamefikia mafanikio makubwa maishani. Ondoa dharau katika nafsi yako amini unaweza. Kuna walioshindwa kama wewe wakadharauliwa na kutemewa mpaka mate… ila walitambua kusudi la maisha yao na leo hii wamefikia mafanikio makubwa sana maishani, kwa nini?? Wewe ukate tamaa na kujidharau katika hali uliyopo ukajiona hauna maana? Hakika unaweza ukiamua,

Mafanikio ni haki yako. 

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA