NINI CHA KUFANYA UNAPOBEBA UJAUZITO WA MWANAUME AMBAYE BADO HAMJAINGIA KWENYE NDOA!

 

iddimakengo 


Najua kila siku huwa naandika kuhusiana na kubeba ujauzito kabla ya ndoa, lakini najua wakati mwingine haya mambo hutokea, mtu atasoma hapa, ataongea na mimi na mwisho atabeba. Sasa kama uko katika hali hii, kwa bahati (sio bahati mabya, hakuna mtoto ambaye ni bahati mbaya, kila mtoto ni bahati hivyo hii ni bahati iliyowahi kabla ya ndoa) umebeba ujauzito.

Umeamua kulea mimba yako, mwanaume ni mpenzi wako,mlikua na malengo ya kuoana, lakini bado muda ulikua haujarika, mtoto amewahi kabla ya ndoa basi kuna vitu vya kufanya. Wanawake wengi wanaoachwa huachwa kasababu hizi tatu, kuna vitu ambavyo ukishabeba ujauzito ni lazima kuviepuka, najua ni ngumu ila usipokua makini na kuacha mambo haya matatu basi unaweza kuishia kuachwa na kuwa single Mother.

(1) Achana kabisa na Kisirani cha kuja kujitambulisha na kukuoa; Najua, neno la kwanza, kitu cha kwanza ambacho hukujia kichwani baada tu ya kumuambia kuwa una mimba yake ni kutaka kujua lini anakuja kujitambulisha kwenu. Wanawake wengi wanapobeba mimba basi huona ndoa, huwa na haraka ya mwanaume kuwaoa na wakati mwingine hata kuja kujitambulisha tu kwakua wanaamini kuwa, kama wasipofanya hivyo mapema basi wanaweza kuwaacha moja kwa moja.

Dada ukiwa katika hali hii hembu pumua kidogo, uliza mipango yake, msikilize vizuri na mpe nafasi ya kutafakari vizuri. Najua nyumbani wanakusumbua, najua unaogopa kuzalia nyumbani, najua unaogopa akikuacha watoto wako watakua na baba tofauti lakini kulazimishia kuja nyumbani kunamfanya mwanaume kukuona kama kisirani.

Wengine wanachanganyikiwa kabisa, mwanaume akionekana haeleweki basi unamtafuta Mama mkwe, dada zake, rafiki zake na kila mtu kuongea naye kama vile hatakuja. Hapana, dada ongea naye mara moja kisha mpe muda, onysha kuwa unajali lakini hujachanganyikiwa, onyesha kuwa pamoja na mimba bado unajipenda, unajithamini. Mna miezi tis aya kusubiri, hii miezi tisa mfanye ajione kama wewe ni mwanamke wa kumpa furaha na si mwanamke ambaye atamsumbua kama akikuoa.
(2) Achana na kisirani cha kuwekeza na maandalizi ya kuhudumia mtoto; Kwa wanawkae hii ni mipango, haya ni malengo ya maisha lakini kwa wanaume hiki ni kisirani. Alikua anakunywa pombe, mnakesha baa au club pamoja, safari za hapa na pale, starehe nyingi. Mwanamke yoyote akibeba mimba atataka mwanaume kuacha haya mambo yote ya kutumia hela hovyo na kuwekeza kwaajili ya kujifungulia na matunzo ya mtoto.

Ni wazo zuri, ni kitu kizuri sana lakini kama kila siku utakua ndiyo wimbo, unalalamika kazi kunywa pombe tu, mara kazi kuhangaika na mrafiki, unatumia pesa vibaya na kumpangia pangia mambo mengine basi moja kwa moja atakuona kama una kisirani, unataka kumkaa kichwani na unaweza kuachwa. Sasa cha kufanya hapa ni nini kama mume haonyeshi kujali na kuwekeza.

Kua mpole, ongea kuhusu mahitaji, kaa naye chini, mpe bajeti ndogo, anza na vitu vya kujifungulia na kisha ongea mambo mengine. Kama unafanya kazi mshawishi mfungue akaunti wote muwekeze kwa pamoja, akipata kidogo anatupia, isimamie kwajili ya mtoto. Nenda naye taratibu, wewe unaogopa kujifungua bila kujiandaa ila yeye anaona ni kawaida, hivyo usimsukume sana kuweka akiba kwani utamsukuma na yeye, utakosa pesa na mwanaume pia.

(3) Achana na watu ambao kila wakati wanakujaza hofu kana kwamba maisha yako yameisha; Wazazi wako hasa Mama yako, Dada zako, marafiki zako, mitandao ya kijamii, kazini, na kila sehemu. Wote hawa watakufanya ujihisi kama vile umakosea maisha, kma ushaharibikiwa, kama ushakufa tayari, kama hutakuja uolewe. Watakuona kama takataka, watataka usione thamani yako tena, yaani ukiwasikiliza utachanganyikiwa.



Dada ushabeba mimba, ni mtoto si jiwe, sio dawa za kulevia hizo kuwa ukijifungua utafungwa. Hapana, ni mimba inaenda kuleta mtoto. Punguza kusikiliza watu ambao wanakukatisha tamaa, hata kama mwanauem haeleweki lakini ukisikiliza hao watu unaweza kujikuta unachanganyikiwa, wanakuchanganya kiasi kwamba unashindwa kujua ushike wapi.

Unakua na kisirani, wanakupa wewe na kwakua huna mtu mwingine wakumpa unampelekea mwanaume. Kila siku ni kulalamika Mama anasema hivi, dada kasema hiki, flani hivi. Mwanaume hata kama likua anakupenda lakini anaogopa kisirani, ahanisi hizo ndiyo tabia zako ulikua unazificha, wengi hata hawajui kama ni mimba hivyo anakuona kuwa hufai kuwa mke wake kwani utambsumbua.

(4) Mwisho nimalize kuwa kisirani pekee kinachohitajimka kwa wakati huu ni kile cha mimba na si cha Maisha. Kisirani kile cha kusema nataka udongo, nataka maembe ya musoma, nataka nazi za mwanza, nataka ndimu ya kokoto. Hivyo wanaume wanavijua, wamevizoea na ni vitamu. Ila visirani vya unakuja lini kujitambulisha, njoo hata wakujue, kama huna mpango basi mpigie hata Mama. Hauko siriasi, huweki akiba na vingine vingi vitayavunja mahusiano yenu kabla ya kuanza.

NB; Kwa wale mliobeba mimba za waume za watu, nyie tayari tu ni masingle mother, kubalianeni na hali komaa tu jamaa ahudumie.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA