NINI CHAKUFANYA KAMA UMEMFUMANIA MKE/MPENZI WAKO ZAIDI YA MARA MOJA NA HATAKI KUBADILIKA!
Kama ukimfumania mwanamke wako na SMS au kiumuona na mwanaume mwingine halafu ukamuonya, ukamuambia kua aachane na huyo mtu basi kama anakupenda na anapata kila kitu kwako ataachana naye. Wanawake mara nyingi hufanya kosa mara moja, tofauti na wanaume, wanawake wana hofu ya kuchika hasa kama wanampenda mwanaume na shetani au ubinadamu ndiyo uliwafanya kukosea.
Lakini kama utamuambia aachane na huyo mtu, labda ni X wake utamuambia kua aache kuwasiliana naye ila bado akaendelea kuwasiliana na huyo mtu basi jua kuna mambo matatu. Kwanza kabisa inawezekana kuna kitu ambacho huyo mwanaume mwingine anampa lakini wewe huwezi kumpa hivyo hawezi kumuacha, inawezekana ikawa ni shughuli kitandani, pesa au hata matumaini ya maisha mazuri.
Pili inawezekana anajua kabisa kuwa kashakukalia na huwezi kumuacha, labda kashakutengeneza kwa watalamu na anaamini kua hata ukimfumania huwezi kumuacha, lakini labda anajiamini kua kuna vitu adimu anakupa huwezi kuvipata kokote au yeye ndiyo mwanaume ndani anakuhudumia kwa kila kitu hivyo anajua kua huwezi kumuacha kwakua huna pakwenda, pia inawezekana anajua kua unampeda sana huwezi kumuacha hata ukimfumania na mwanaume mwingine.
Jambo la tatu inawezekana huyo mwanaume mwingine kamdanganya sana kua hata akiachika basi anamuoa yeye au ataishi naye, wanawake ni watu wa kuamini wanaume hasa ma X wao, au masponsor wao hivyo kama kaambiwa hivi na wewe hakupendi sana wala hatajali, tena hapa ndiyo anaweza kuwa anafanya mambo mengi waziazi ili ugundue na umuache, au anataka kukuonyesha kuwa wewe si lolote si chochote.
Utafanya kosa kubwa kama ukimfumania mara ya pili na ya tatu ukaenda kwa ndugu zake, wadhamini wa ndoa, rafiki zake anaowaamini au mtu yeyote ili kuongea na mwanamke wako. Utafanya kosa zaidi na mwanamke atakuona fala wa mafala, narudia atakuona fala wa mafala kama utachukua simu yako na kumpigia mwanaume mwenzako, mtu ambaye anatembea na mpenzi wako au mke wako na kumuambia aachane naye.
Hata kama ni msataarabu na atachana naye lakini mke wako hataacha kuchepuka, mwanamke ambaye umeenda kumuombea kibali kwa mchepuko wake ili aachwe kamwe hataacha kuchepuka, anaweza kuachwa kwakua huyo mwanaume mwingine alishamchoka au hataki maneno lakini kwakua kichwani kwake mwanamke anaona kama kashakukalia basi nilazima atatafuta mwanaume mwingine, ataendelea kuchepuka kwani atazidi kukudharau na anajua kua huwezi kumuacha.
Kama unataka mwanamke abadilike kweli ni lazima uwe na ujasiri wa kumuacha, sisemi kauchana naye moja kwa moja hapana. Kama ni mpenzi wa kawaida, unapomfumania, unapomuona anarudia kosa lle lile kwa mara ya pili, kama alikua na vitu vyake kwako mpelekee na muambie kwa heri. Ataondoka na mpe kama miezi mitatu, lakini kama ni mke wako wa ndoa, wakati akitegemea utaita wazazi, ndugu na hata mshenga mrudishe kwao na wakabidhi mtoto wao.
Kama unaishi kwake, wewe ndiyo umewekwa kwake, chukua vitu vyako katafute chumba kwingine na muambie kabisa kama mna watoto kua mtalea watoto. Hapa unakua unafanya mambo mawili, jambo la kwanza nikua unamfundisha kua huwezi kuvumilia ujinga wake kila siku, huwezi kuishi naye kama bado ataendelea kuwasiliana na hao watu wake. Lakini jambo la pili unampa nafasi ya kutambua umuhimu wako, wakati alitegemea labda utampiga, vitisho na kukasirika jitenge naye ili ajue umuhimu wako.
Kama itapita miezi mitatu na hatataka kurudi kwako na kuomba msamaha basi jua kua wewe mwanaume ndiyo ulikua na matatizo na kuchepuka kwake ni kwakua alishakuchoka. Iko hivi, wanawake wengi huchepuka kwa kudanganywa, huchepuka kwa kudhani kua michepuko inahudumia zaidi, inajua mapenzi zaidi, haina kelele kama mume na huona kama inapedwa zaidi na michepuko kutokana na vizawadi pamoja na kujali ambako waume zao hawana.
Kitu ambacho hawajui nikua mchepuko unahudumia vitu vidogo vidogo tena vile vyakijinga wakati mume au mpenzi mkuu huhudumia mambo ya maana. Wakati mume anahudumia chakula, mchepuko unamtoa out kwa Dinner, wakati mume anahudumia mavazi, mchepuko unanunua maua, wakati mume analipia ada, mchepuko unalipia vacation, wakati mume analipia kodi ya nyumba mchepuko unalipia Hoteli.
Kwa maana hiyo basi ukimuacha, ukamrudisha kwao mchepuko utakiambia kwani nao unamajukumu yake, kwamba tayari ana mtu wake ambaye anamtimizia majukumu yake hivyo hawezi kubeba gharama za kumlipia kodi, kumpa chakula, kumhudumia matibabu. Wanaume wengi wanaotembea na wake za watu wakishajua kaachika wanajua kua kashakua mzigo hivyo wanakata kabisa mawasiliano, hakuna mwanaume mwenye akili zake atabeba mzigo wa mwanaume mwingine.
Kwa maana hiyo katika kipindi ambacho utamuacha, kipindi ambacho hutakua na mawasiliano naye, kipindi ambacho utakua unahudumia watoto tu basi mwanamke ataamka na kujua kua kumbe wale waliokua wanamdanganya hawawezi kumpa furaha kama mume wake, kwamba walikua wakibeba majukumu madogo madogo kuliko mume ingawa yeye alikua akiyaona ya muhimu.
Mwanamke wa namna hii ambaye atakua kashapigika kwao, ndugu hawamtaki, mchepuko haumtaki hata kama ana kazi yake lazima akukumbuke kama kweli na wewe ulikua mwanaume kweli. Kama na wewe ulikua ni mwanaume Boxer, ulikua hubebi majukumu yako ya chumbani au ya kuhudumia familia kama mwanaume basi hatakukumbuka, sanasana atashukuru Mungu umemuacha ili aanze upya, ukiona umemrudisha miezi sita hata harudi kuomba msamaha basi huna hata haja ya kumrudia.
Kwanza jua hakupendi, alikua anakuvumilia tu pengine kwasababu ya watoto, alishachoka tabia zako na ujinga ujinga wako mwingine. Anafuraha huko aliko, hivyo wewe ndiyo ulikua na matatizo, ongea naye jirekebishe ndiyo umrudie. Lakini kama akirudi na kuomba msamaha basi hembu angalia mapungufu yako jirekebishe na msamehe, kuna mwingine ataomba msamaha kwakua hana pakwenda lakini bado una tabia za hovyo huyu atarudi lakini bado ataendelea kuchepuka.
Lakini kama tatizo ni yeye, alikua anadanganywa danganywa tu basi jua akikuomba msamaha akirudi kwako atakua kajifunza. Ila kama kila siku utakua ni kulalamika, kulalamikia mashoga zake, ndugu zako, ndugu zake basi jua hatabailika, hataacha kwuasiliana na X wake, hataacha kuchepuka na yule mume wa mtu. Hata kama wewe si mdhaifu kwake lakini atakuona mdhaifui na kuhusu kuwa huwezi kumuacha, na ikiendelea hivyo jiandae tu kulea watoto wa watu.