DALILI KWAMBA MCHUMBA WAKO ATAKUA KITASA (MBAHILI) NA HATA KUFIKIA HATUA YA KUKUACHIA ULEE WATOTO MWENYEWE!
Najua Dada zangu mnapokua mnapenda kuna vitu vingi ambavyo hata hamviangalii, yaani kuna mapungufu mengi mnaona kama ya kawaida tu na mnasema mtakabiliana nayo mbele kwa mbele. Kwa mfano uko na mwanaume ambaye hata hela ya Bajaji kwenda kwake hajawahi kukupa. Unaenda kwake kumfulia, kumpikia na kutumika lakini hata nauli hakupi!
Unajipa moyo akikuoa ukiwa mkewe atabadilika, nikweli wengi hubadilika, hii ni kutokana na ukweli kua wanaume wengi huona kama ni ufala kuhudumia mchumba au mpenzi wa kawaida lakini huona kama ni ufahari kuhudumia mke. Kwa maana hiyo wakati wa uchumba anaweza kuwa mbahili ila akaja kubadilika baada ya ndoa na kubeba majukumu yake kama mwanaume.
Lakini pia kuna wengine hawawezi kubadilika kirahisi na huhitaji nguvu ya ziada. Sasa ukiacha na ule ubahili wa kawaida, kuna tabia ambazo mwanaume wako akikuonyesha basi ujue hiyo ni Kengele, huo si ubahili wa kawaida unahitaji kusoma makala yangu nyingine kujua namna ya kuishi naye kama akikuoa, hembua angalia tabia hizi.
(1) Anakuacha Ulipie Chakula Mkitoka; Mwanaume atakua mbahili mpaka basi katika kukupa hela lakini anajua kua jukumu la kulipia bili na hata chumba cha kufanyia mambo yenu ni lake. Kama mwanaume unatoka naye na karibu kila siku bili unalipia wewe na wala hajali ndiyo kwanza anajisifia kuwa ana mpenzi mtafutaji huyo kuwa naye makini, atakutelekezea hata watoto.
Kuna wale ambao mnatoka na wanafunzi unajua ni hohe hahe au tuseme hana pesa, hapo sishangai sana, lakini naye hata siku moja moja ataona aibu alipie. Ila kama ni mwanaume, ana kazi yake halafu mnatoka, bili inakuja hata hajikuni anakuacha unalipa, Dada yangu hapo ni kukimbia tu. Ukiwa mwanaume una DNA za kiume utaona aibu na utalipa na hutafurahia kula bure kila siku.
Akijitahidi sana atakuja na Ndizi na mara moja moja ka kilo ka nyama ndiyo ntolee. Huyo Dada yangu ni mzigo anakuja kwako kula tu, anaweza hata asikuoe na hata akikuoa ni majanga kuwa makini naye. Nilazima mwanaume hata kama anakuja kwako kula, basi yeye ndiyo atoe hela ya chakula, tena acha kupikia mkaa anunue na gesi kabisa na kama hatoi hela ya kula, dada hembu anza Diet, usimfukuze, ila siku anakuja kakuta umekatakata matunda wala huna wasiwasi!
Najua kwakua unatamani ndoa unadhani ukimpikia ndiyo atakuona ‘Wife Material’ dada wife wanapika vyakula vilivyoletwa na mume na si kutafuta mwenyewe. Hivyo hembu pika vichips mshenzi vyako vitatu halafu ametoka kupiga chuma huko wala usimnyime mkaribishe aone aibu hata anunue, ila ukimuendekeza basi jua hata akikuoa unaenda kuumiza viungo vyako vya uzazi tu!
(3) Anaanza Kulalamika Kila Siku Hata Kama Hamzungumzii Mambo Ya Hela; Kitu cha kwanza anapokuona tu ni kulalamika kuhusu kazi, pesa, alivyorushwa, madeni, majukumu na mambo mengine. Yote hii ni ili usimuombe pesa, umuonee huruma na kumuona masikini na hata umsaidie kitu flani ndugu yangu huyu ni majanga balaa kuwa naye makini. Yaani hawi hata kama wanaume wengine azungumzie mpira.
Yaani yeye hata hili suala la Arsenal kufungwa kila siku halimuumi yeye ni kulalamika kuhusu bosi wake, mara kadhulumiwa posho, mara ada za wadogo zake, mara kodi ya nyumba. Meseji umemtumia vipi umeamkaje anaanza kukuambia kua hajanywa chai utafikiri unauza Mama Lishe! Dada yangu kama una wa namna hiyo basi jua unaenda kujioa, kujihudumia, kujilisha na kulisha hata ndugu zake.
(4) Anakuomba Hela Na Anakasirika Usipompa; Yes Mama umpenzi tu lakini kila siku anakulilia shida anaomba vielefu kumi kumi, vocha na vitu kama hivyo. Yaani yeye hajawahi kukupa hata kumi ila yeye nikuomba tu kila siku, na ukisema huna anakununia wiki nzima kama umemuibia bwana, utasikia “Ohhh wewe utakua hunipendi!” Huyo hata siju ni kwanini bado uko naye, ni mzigo tu na unabeba mateso! Hakuna mwanaume wa hivyo huyo ni wa kiume na hana tofauti na Dada yako!

Lakini na wewe ni fala, narudia wewe ni fala hivi utakua unampaje mwanaume hela kila siku? Unanunua ndoa? Eti kisa anakasirika, hata kama hana si akakope kwa wanaume wenzake huko kwani hao wengine wanaodaiwa wamepungukiwa nini? Dada yangu kama uko na mwanaume, anakuomba hela na usipompa basi anakununia basi huyo anakupotezea muda hembu acha kumpa kama hutaona anakukimbia, ni kichomi!
(5) Ukimuomba Hela Anajifanya Kukasirika Na Hakutafuti; Umemuomba hela kidogo ananuna, mara unapenda hela, sijui huna mapenzi ya kweli yaani anataka ujisikie vibaya ili uone kama umemkosea, ujione kua unapenda pesa na msamaha uombe. Yaani elfu kumi tu ananuna wiki nzima mpaka umuombe msamaha, kama ana tabia hii huyo ni tatizo, kua makini naye utakua unamhudumia wewe.
Achana na wale akina dada ambao mnaomba hela kila siku, ambao mmeshaua mpaka ma bibi zenu ambao walikufa kabla hamjazaliwa? Hapana siwazingumzii hao, nazungumzia wale amabo umeomba tena mara moja kwa kumjaribu lakini analalamika kana kwamba umemuambia akununulie Gari kumbe umeomba hela ya Bodaboda ili uende kwake! Kama una wa namna hiyo anza kujipanga tu kwani inawezekana hata wewe si mpenzi wake ni mchepuko tu!
(6) Anakutuma Kuomba/Kukopa Kwa Wengine Kwa Shida Zake; Ndiyo ukiwa huna yaani anajua mpaka pa wewe kuzipata, utasikia si uongee na Kaka yako, muambie Bosi wako, yule rafiki yako hawezi kukukopesha, Mama yako atakupa. Baba yako ankaupenda atakupa. Yaani huyo ni mwanaume kakuomba hela umesema tu huna na anajua huna lakini badala yeye akakope anakutafutia na sehemu za kukopa.
Ni kama anakuchuna flani na analazimisha uwe na hivyo vitu. Ndugu yangu kama unakutana na mtu wa namna hii basi jua umeingia mkenge, huyu ni kero akikuoa anaweza hata kuuambia uende kuchukua chakula nyumbani kwenu. Kuwa makini sana na mtu kama huyu kwani ubahili wake si wa kawaida. Sasa najua huwezi kumaucha kwani umemsumbukia sana.
Unataka kujua ni namna gani ya kuingia kwenye ndoa na mtu wa namna hii, kwamba ninamna gani utamlazimisha kubadilika na angalau asije kukutelekezea watoto basi karibu angalia Makala inayofuata. Lakini usisahau kusoma kitabuchangu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu”. Ni shilingi elfu kumi