ACHA KUWA MTUMWA WAKE KWA KUBEMBELEZEA NDOA UNAWEZA USIIPATE AU UKAPATA YA MATESO!
Umekua kama roboti, kama huna akili zako, unaona anafanya maamuzi mabovu tena yanayokuhusu lakini husemi, kwakua unabembelezea ndoa unaamini kua mke bora ni kukubali kila kitu basi unakubali. Unamuacha anakupangia mpaka maisha yako, huwezi kuamua nifanye nini unamsikiliza yeye tu, akikukataza kitu huulizi hata kwanini unafuata tu, ndugu yangu hapo unatengeneza mwanaume ambaye atakukontrol kwa kila kitu.
Mwanaume ambaye atakukataza kufanya kazi, kuenda sehemu, na ambayo hatataka ujue mambo yake. Hivyo kua makini wakati huu, mambo mengine muambie hapana apate ujumbe kuwa ukiwa mke hutakua unafuata kila kitu bali utakua na akili zako, hutapelekeshwa. Najua wanawake wengi mnapokua katika kipindic ha uchumba mnaogopa, lakini tambua kuwa wewe ni binadamu si Roboti.
Kiuhalisia nikuwa kila mwanaume anahitaji mwamke ambaye atamuambia hapana hata mara moja moja hasa katika mambo ya muhimu. Unapokua unakubal I kila kitu anachokufanyoa bila kuhoji wakati wa uchumba basi jua kuwa wakatoi wa ndoa utakua ni wale wanawake ambao mume anajenga lakini hujui hata kiwanja kiko wapi achilia mbali kina jina la nani?
Unatakiwa kujua kuwa wewe si bidhaa una maoni yako, hata kama hatayasikiliza lakini unayo. Lakini mchumba wako si mume wako, hawezi na wala hapaswi kukupangia mambo hasa ya muhimu, anaweza kukukataza kuvaa kimini na kupiga picha za uchi lakini kamwe usimuelewe kama akikukataza kusoma, kufanya kazi au vitu vingine vya maendeleo. Hata kama unafanya biashara na mtu falani ambaye yeye hampendi ilimradi si mumeo hawezi kukukataza.
Wanawake wengi sana hujitoa wakati wa uchumba kiasi kwmaba hata ikifika katika ndoa wakati ambao walidhani kama wanaweza kupumzika kunakua hakuna kitu cha kupumzika. Mateso yanaongezeka kwakua ulishamzoesha mwanaume kukufanya mtumwa, acha kukubali utumwa kisa unabembelezea ndoa, kuna mambo mawili, unaweza usiipate hiyo ndo aunayobembelezea au ukaipata lakini ya mateso!