BADO NATAFUTA - SEHEMU YA 03

BADO NATAFUTA
Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 04
WhatsApp:0678926045
Tumehangaika sana sisi kupika wakati huos gril upo na umeenda kutembea mjinga we we, aliongea mama yake mdogo wa mniga huku akamvutia ndani mniga harafu akafunga geti,
'"Bamdogo nisamehe kama nimekosea ila Mimi nilienda kwa rafiki yangu john kumtembelea, aliongea mniga huku bado anatetemeka sana hata kabla baba heppy hajaongea Mara mkewake akadakia na kumwambia mumewe,
"'Unajuwa mume wangu mniga anafundishwa kuvuta bangi na huyo john ndomaana sikuizi kawa jeuri kweli yani, aliongea mama heppy,
'"Oh kumbe ndomaana hata hapa nikimtazama naona macho yake mekundu sana kumbe anavuta bangi sasa Leo atanitambua huyu kinyago, aliongea baba heppy na kuchomoa mkanda wake kwenye suruale na kuanza kumtandika mniga popote tu,
'"Uwiiiiiiii bamdogo nisamehe nimekoma Mimi jamaniiii, mniga akashindwa kuvumilia na alianza kulia kwa sauti sasa,
'"Hakuna kumsamehe mume wangu maana mtoto huyo atatushinda mtandike sana tu, aliongea mama heppy na kuzidi kumpa kichwa mumewe ambae alikuwa anamtandika sana mniga na mkanda wa suruale,
'"Bamdogo nisamehe nimekosa sirudii tena, aliongea mniga huku anaendelea kupokea tu kichapo,
'" hakuna nikusamehe nini mtoto unakuwa jeuri sana yani unaenda kushinda kwa john unaacha kutupikia sisi chakula Leo utaniambia, aliongea baba heppy huku akiendelea kumpiga mniga ambae alikuwa tu analia Mara alikuja Estar ambae alikuwa kashika fimbo kubwa kweli na kumwambia,
'"Baba chukua hii ndo ataumia vizuri kuliko mkanda huo haumii maana hapo anakuigizia tu kulia, aliongea Estar
'"Safi sana mwanangu maana kweli huu mkanda haumizi naona, aliongea baba heppy na kuchukua fimbo ili amchape sasa ile anataka kumchapa tu Mara fimbo yake ikadakwa na mtoto heppy ambae alimwambia,
'"Baba sasa huo ni uonevu maana umempiga sana mtoto wa watu ila katulia kimya kwani unafikili kwa umri alionao anashindwa kukupiga au ila tu anakuheshimu basi na wewe muheshimu bwana sio kumtesa tu mtoto wa watu kisa mpole, aliongea heppy kwa uchungu sana huku machozi yakimtoka,
'"Mkewangu huyu mtoto kaingia nini lakini hadi ananikosea heshima na kuja kushika fimbo yangu ntamfumua Mimi sitojari mwanangu, aliongea baba heppy kwa hasira sana,
'"Kama unanipiga nipige ila tu muache mtoto wa watu maana mmempiga sana kaa niko tayali kubeba azabu yake na baba kwanini unashindwa kuwa na huruma na mtoto wa kaka yako kumbuka hizi mari ni za baba yake, aliongea kilefu tena heppy na kumfanya baba yake azidi kukasirika sana,
'"Kwani wewe mtoto unakichaa ee sasa ngoja nikufunze adabu, aliongea baba heppy na kutaka kumpiga heppy ambae hakukimbia wala nini,
'"Mume wangu jamani msamehe tu mtoto wetu maana utamuumiza bule, aliongea mama heppy
'"Sawa nimekuelewa mke wangu wewe mbwa mniga nenda jikoni katupikie chakula huko, aliongea baba heppy na mniga akatoka mbio hadi jikoni huku anasikilizia maumivu ya mkanda aliopigwa nao, akaanza kupika huku kichwani kwake akijisemea,
'"Yani hapa ndo kila siku ntakuwa naenda hadi nipate pesa ya kwenda kupanga chumba changu nimechoka manyanyaso yao, alijiwazia mniga na kuendelea kupiga hadi chakula kikaiva na akaenda kutenga ,

Kwa 1500 tu unajipatia story hii mbaka mwisho lipia kupitia Tigo Pesa 0678926045 au Halo Pesa 0620816989 ukilipia ntumie ujumbe Facebook Inbox na WhatsApp)

Itaendelea...............

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA