BADO NATAFUTA SEHEMU YA 03

BADO NATAFUTA
Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 03
WhatsApp:0678926046
Hapana bwana wewe mtoto mchawi maana nimekutuma sasahivi na wakati sijakupa pesa ya bodaboda, aliongea mama yake mdogo wa mniga
'"Kweli Mimi sio mchawi na nilimevileta vitu vyote bosi, aliongea mniga
'"Sawa kama ndohivo kunanguo zipo nyuma kule kafuwe maana wanangu kesho j,pili inatakiwa twende bauch tukale raha tu, aliongea tena mama yake mdogo
'"Duuh bosi kwa sasa nimechoka sana naomba nikapumzike kesho ntazifua bosi wangu, aliongea mniga kwa huruma kweli yani,
'"Weeee mbwa unasemaje nimekwambia Mimi kafuwe haraka staki kubishana na kinyago wewe shenzi kabisa, aliongea kwa sauti Kali mama heppy na kumfanya mniga atetemeke kidogo,
'"Sawa bosi ntaenda sasahivi kuzifuwa, aliongea mniga na kuondoka huku kakasirika kinoma yani alitamani hata kumpiga vibao, ila ndo hivo tu akazunguka hadi nyuma ya nyumba akakuta furushi la nguo hadi nyingune zilikuwa safi ila tu nikumkomesha hapo mniga akakumbuka msemo wa wahenga usemao,
'"Akufukuzae hakwambii toka, sasa mniga yamenikuta, aliwaza sana mniga ila akaanza kufua kwa haraka sana ingawa lilikuwa rundo kubwa sana kwanzia saa kumi jioni hadi saa moja ucku ndo akamaliza huku kachoka sana yani, akajikokota hadi sebleni akamkuta baba yake mdogo na wanae huku mama yake mdogo nae yupo,
'"Ehee mniga unatoka wapi sasahivi ucku nyani wewe, aliongea baba yake mdogo,
'"Nilikuwa nafua nguo alizoniambia mamdogo, aliongea mniga, Mara mama yake mdogo akadakia,
"'Weeee nikane mtoto wewe ulikuwa na Mishe zako unisingizia Mimi, aliongea mama yake mdogo
'" Oh sasa unasikiwa wewe mniga kwahio sasa uongo umepitiliza sio ukaamuwa kunidanganya, aliongea baba yake mdogo huku kamkazia macho mniga,
'"Kwahio mama mdogo sasahivi unanikana sio sasa Mimi nasema kwanzia Leo usintume tena, aliongea mniga kwa hasira sana hadi kila mmoja pale sebleni akamuangalia mniga maana kwakuwa mweupe sasa rangi ikabadilika akawa mwekundu,
'"Wewe nije nikusikie kakutuma huendi ndo utantambua hapo kwamba Mimi ni nani, aliongea baba yake mdogo, Mniga hakujibu kitu chochote bali alienda zake chumbani kwake na kujiraza huku machozi yanamtoka tu hadi usingizi ukampitia ingawa ulikuwa wa mang'amu ng'amu, kulivo pambazuka tu mniga aliamka na kuanza kufanya usafi kama ilivokuwa kawaida yake alivomaliza tu kwakuwa mabosi bado wamelala yeye akaondoka zake mdogo mdogo hadi kwa john rafiki yake ambae alimkuta nae ananawa uso,
'"Duuh jamaa yangu unamichare kinoma yani maana nilitaka nikufate sasahivi yani, aliongea john
'"Daah ingekuwa kesi maana tayali wakina bamdogo wangenizingua tena, aliongea mniga
'"Oh haa nilisahau siunajuwa kazi asubuhi bhana sasa nimeona kama utachelewa vile, aliongea john
'"Hapana sasa kwanza tunaenda kupiga mishe gani labda, aliongea mniga
'" Mishe yenyewe jamaa yangu ni kwenda kuchimba mtaro kwa mama Sara, aliongea john,

Kwa 1500 tu unajipatia story hii mbaka mwisho lipia kupitia Tigo Pesa 0678926045 au Halo Pesa 0620816989 ukilipia ntumie ujumbe Facebook Inbox na WhatsApp)

Itaendelea................

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA