BADO NATAFUTA SEHEMU YA 02

BADO NATAFUTA
Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 02
WhatsApp:0678926045
Aliongea mama yake mdogo huku anamvuta shavu mniga,
'"Nimekwambia kwanzia Leo Mimi usiniite mama yako mdogo niite bisi hadi hapo nazani utakuwa umenielewa, aliongea tena,
'"Nimekuelewa bosi wangu ntakusikiliza usemacho, aliongea mniga huku anataka kulia kabisa,
'"Hapo sawa sasa nisikilize kwa makini sana inatakiwa uende sokoni ukanunue mshele kilo kumi na maharage kilo kumi mafuta ya kupikia lita kumi na uniletee hapa sasahivi olewako uchelewe ndo utantambua kwamba Mimi nani, aliongea mama yake mdogo, mniga alihesabu hella alizipewa na kukuta zimeenea ila kasoro ya bodaboda,
'"Nimekuelewa bosi ila sasa hela ya bodaboda yakubebea mizigo mbona nipe, aliongea mniga,
'"Weeee mpumbavu nini kwani wewe unakazigani mbaka usibebe mizigi hiyo au unanichokoza wewe mbwa, aliongea mama yake mdogo kwa ukali kweli,
'"Hapana bosi ila kule mbali na vitu umeniagiza ni vizito, aliongea mniga kwa huruma kweli,
'"Nakwambia wewe endelea kusimama hapo nikamwambie mwenzako aje akunyuke maana naona bado hujatisheka, aliongea mama yake mdogo huku akinyanyuka,
'"Nisamehe bosi wangu naenda usiende kumwambia, aliongea mniga na kuondoka zake huku yupo mbio mbio ili awahi maana kachoka sana, alikimbia ila wakati yupo njiani akapata wazo la kwenda kwa rafiki yake john maana kwao wana baskeri, hapo alikimbia hadi nyumbani kwa kina john kwa bahati nzuri akamkuta john anachezea baskeri hapo ndo ikawa rahisi kwake,
'"Oi john niambie jamaa yangu, aliongea mniga,
'"Oh safi Mishe vipi, aliongea john,
'"Daah safi ila nilikuwa na shida jamaa yangu sijuwi utanisaidia, aliongea mniga kinyonge kweli,
'"Wewe sema ikiwa iko ndani ya uwezo wangu ntakusaidia, aliongea john,
'"Nilikuwa naomba msaada wako wa baskeri ili ikanisaidie kubeba vitu nilivo agizwa na mama mdogo, aliongea mniga,
'"Duuh kumbe swala lenyewe ndo hilo ila unajing'ata kusema jamaa yangu haya panda twende nikukimbize fasta, aliongea John na kumfanya mniga afurahi sana, safari ikaenda hadi sokoni na mniga akanunua mahitaji alioagizwa alipomaliza wakapakiwa kwenye basker na john akaanza kuendesha kwa speed mniga anakimbia tu hadi wakafika jirani na nyumba ya kina mniga ndo john akasimama,
'"Duuh jamaa yangu asante sana maana nilikuwa nawaza ntabebeje mizigo yote hii ila umenisaidia kinoma yani, aliongea mniga,
'"Usijari mshikaji wangu Mimi na wewe tumetoka mbali sana tangia utotoni bhana, aliongea john,
'"Sawa sasa ngoja nisombe mmoja mmoja kwanza, aliongea mniga na kupeleka mchele jikoni akaja akabeba tena maharage hadi vyote vikaisha hapo akamrudia john,
'"Oi sasa ngoja nirudi nyumbani na kesho uje tukapige ishu jamaa, aliongea john,
'"Oh sawa hakuna noma mchizi wangu, aliongea mniga na kuagana huku mniga akirudi ndani moja kwa moja hadi alipo mama yake mdogo na akamwambia,
'"Bosi tayali nimesha nunua na vitu viko ndani, aliongea mniga,
'"Umesemaje wewe mtoto inamaana sasahivi umerudi tayali au unantania, aliongea mama yake mdogo,
'"Hapana sikutanii ila nimekuja navo, aliongea mniga,
'"Hapana bwana wewe mtoto mchawi kabisa haiwezekani sasahivi uwe umerudi bhana, aliongea mama yake mdogo,

Kwa 1500 tu unajipatia story hii mbaka mwisho lipia kupitia Tigo Pesa 0678926045 au Halo Pesa 0620816989 ukilipia ntumie ujumbe Facebook Inbox na WhatsApp)

Itaendelea...............

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA