CHOMBEZO: BADO NATAFUTA SEHEMU YA 5

BADO NATAFUTA
Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 05
WhatsApp:0678926045
Yani hapa ndo ntakuwa naenda kila siku tu, alijiwazia mniga na kuendelea kupika hadi chakula kikaiva na alipomaliza tu, alijipakulia kwanza yeye akala haraka haraka na alivotosheka tu ndo akaenda kutenga mezani ambapo mabosi walikuwa wamekunja nne tu,
"'Kalibuni chakula tayali kipo mezani, aliongea mniga kwa sauti ya chini kweli,
"'Oh asante sana hayo ndo maneno bhana ili sisi mabosi wako tusipate shida ya kupika tena hahahahaa, aliongea baba yake mdogo wa mniga, huku wakielekea mezani na kuanza kula kwa furaha sana, kulivokucha tu mniga fasta aliamka na kufanya usafi maeneo yote ya nyumba na alipomaliza tu akaelekea jikoni na kuwapikia chai ilivoiva fasta fasta akawatengea mezani yeye akatoka mdogo mdogo hadi kwa rafiki yake john ambae alimkuta anaongea na simu, alimsubili hadi pale alipomaliza ndo akamsalimu,
'"Niambe john uko poa kabisa, aliongea mniga
''Sana tu sijuwi wewe mchizi wangu, alijibu john
'"Nipo guda tu vip mishe wapi Leo jamaa, aliongea mniga,
'"Daah Leo tunaenda kwenye kushona mahindi kwenye ghara la bosi musa ambae anamashine ya kukoboa na kusaga unga wa sembe, aliongea john
'"Duuh nibonge la ishu kinoma yani jamaa sasa kakwambia shingapi kujaza kushona na kuingiza ndani, aliuliza mniga,
'" yeye kaniambia kazi yote anatupa laki tatu jamaa yangu, aliongea john,
'"Duuh kumbe mkwanja mlfu sana kwani yapo kama gunia ngapi, aliuliza mniga
'"Aliniambia zipo kama gunia mia mbili, aliongea john
'"Duuh jamaa mbona kama mahindi mengi sana, aliongea mniga
"'Ndio hivo ila sasa mimi nataka tukafanye kazi sisi wawili tu mwanangu, aliongea john,
'"Kweli kabisa na tukimaliza hapo Mimi inatakiwa nikapangishe chumba changu nimechoka manyanyaso kule, aliongea mniga
'"Sawa hakunashida twende zetu na wakati wa kurudi Mimi ntapitia kwenye nyumba ya mama jeni nimuulize shingapi chumba kwa mwezi, aliongea John na kumfanya mniga afurahi sana safari iliendelea huku wanapiga story hadi wakafika na mniga alishangaa kuona ni bonge la rundo ya mahindi,
"'Duuh mwanangu inatubidi tufanye kazi kwa bidii sana, aliongea mniga
"'Usijari mwana, alijibu john na kazi ikaanza ya kupiga dawa mahindi na kuyajaza kwenye mifuko ndo ilikuwa kazi yani kutoka asubuh hadi inatimia saa moja usiku ndo wanamaliza kupiga dawa na kuyajaza,
"'Aisee dawa Kali kweli hii jamaa inabidi tukapate maziwa ili kesho tukija ni kushona na kuingiza ndani yani, aliongea john
'"Kweli maana hapa nilipo nimechoka kinoma yani hata stamani tena kuyashika madawa, aliongea mniga,
'"Hahahaha jikaze mtoto wa kiume unazani pesa inapatikana kiuraini tu, aliongea john na kumcheka mniga,
'" nalitambua hilo ila duuh jamaa hatali sana sasa ngoja Mimi niwahi nyumbani wewe pitia kule kwenye nyumba basi, aliongea mniga
'"Poa hakunashida Mimi ntaenda ila tu kesho asubuhi inatakiwa uwahi ili tumalize mapema kushona ili tuingize, aliongea john
'"Sawa hakuna noma, aliongea mniga na kuanza kukimbia kuelekewa nyumbani kwao huku anapanga mbinu ya kumdanganya baba yake mdogo, hakuchukua muda sana alifika na kukuta geti limefungwa ikam,bidi agonge huku akisubili majibu Mara kidogo likafunguliwa na heppy ambae alimsalim,
'"Shikamoo kaka mniga, aliongea happy
'"Marahaba mdogo wangu vipi baba na mama wapo, aliongea mniga
'"Ndio wapo tena wanakusubili kwa hamu kweli kaka yangu sijuwi watakupiga kama sikuile, aliongea happy kwa sauti ya chini sana yenye huzuni kama anataka kulia vile,
'"Usijari mdogo wangu Mimi nimejipanga kwa lolote tu wala usihuzunike, aliongea mniga na kumkumbatia heppy
"'Sawa kaka Mimi ntakuibia chakula na ntakuletea chumbani kwako, aliongea heppy huku anafunga geti na kuongozana na mniga mdogo mdogo hadi ndani sebleni ambapo walipokelewa na kwa kuambiwa,
''"Heppy umemtoa wapi huyu nyangau ambae hasikii nilimwambia nini Jana sasa Leo atanikoma, aliongea baba heppy kwa hasira sana,

Kwa 1500 tu unajipatia story hii mbaka mwisho lipia kupitia Tigo Pesa 0678926045 au Halo Pesa 0620816989 ukilipia ntumie ujumbe wa muamala Facebook Inbox au WhatsApp)

Itaendelea.................

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA