KAMA KILA SIKU UNALALAMIKA HUPATI HUPATI WANAUME SIRIASI BASI SOMA HAPA



Hili ni lalamiko la wanawake wengi, hapa iwe ulikuwa unatembea na mume wa mtu au la. Unapoachana na mtu uliyedumu naye kwa muda mrefu, au unapomaliza utoto wanawake wengi huanza kutafuta wanaume ambao ni siriasi.

Sasa labda niwaambie tu kitu kimoja, hakuna wanaume wa namna hiyo. Yaani mwanaume anakutongoza siku ya kwanza anaonesha yuko siriasi anataka kuoa huyo ni muongo.

Lengo la kwanza la mwanaume la kutongoza kwa walio wengi ni kufanya mapenzi basi. Ndoa na usiriasi huja baadaye na si baada ya siku mbili tatu. Hivyo usidhani kwakuwa kakuambia nataka kuoa, kakuambia kachoka kudanga na hivyo anamaanisha.

Wanaume wengi siku hizi wanajua kuwa wadada wengi wanapenda ndoa hivyo wewe ukishamlalamikia kuwa umeumizwa sijui unataka mtu siriasi na yeye atakuambia anataka kuoa. Wengine ni washenzi zaidi ataenda hata kukutambulisha kwa dada yake na shangazi au marafiki.

Lakini lengo ni lile lile kukutumia basi. Sasa hembu acha kutafuta mwanaume siriasi kwani hayupo, tafuta mwanaume anayekufaa. Hapa nikimaanisha kuwa angalia muonekano wake je ndiyo unaoutaka, angalia namna anavyokujali, si kutoa hela hapana anavyojali hisia zako.

Angalia namna anavyokuheshimu kama mwanamke na mambo megine ya nje. Kama yote hayo ni sawa basi furahia mahusiano, usisukume ajenda ya ndoa au kuwa siriasi mapema. Iko hivi miezi miwili ya kwanza uliyopo na mwanaume wako mpya anakuwa bado hajamalizana hata na mpenzi wake wa zamani.

Najua unashangaa lakini usidhani kuwa mwanaume akikutongoza basi alikuwa single hapana ana mtu tayari hata kama si siriasi lakini yupo. Hivyo wewe angalia je huyu tutaendana kama mtaendana basi huo usiriasi utapatikana katikati mkishasomana tabia.

Lakini kama ukitaka siku ya kwanza awe siriasi, aanze kukujali siku ya pili, akutreat kama galfriend siku ya nne basi utatafuta sana na hutampata. 

Utajiona kama huna bahati labda unamikosi kumbe una haraka tu, punguza spidi utaona namna hao ambao hawako siriasi wakikuona unajielewa atakuwa siriasi.

Ondoa presha ya kutaka kuolewa na kutaka kupata mwanaume ambaye yuko siriasi. Hapana huyo hayupo tafuta mwanaume ambaye unamtaka, kwamba akikutongoza angalia kama ana vigezo vyako, hicho cha usiriasi ni cha baadaye sana.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA