Hawa Ndio Maadui Wakubwa Wawili Wa Uchumba Au Ndoa Yako.


......
Miongoni mwa matatizo mengi ambayo yanayowasumbua watu moja ni mapenzi lakini watu bado hawajagundua nini chanzo cha matatizo haya. Kuna watu wanateseka sana na kupata taabu katika uhusiano wao wa kimapenzi mpaka watu wengine wanaamua kuapa na kusema hawataki kusikia kitu kinachoitwa mapenzi hii ni baada tu ya kutendwa vibaya au kusalitiwa na mwenzi wake.

 
Katika safari ya mapenzi kuna mambo mawili ambayo ni uchumba na ndoa. Kabla hatujaanza kujua kiini cha matatizo ya ndoa au uchumba tuangalie kwanza nini maana ya ndoa na uchumba.
Uchumba ni mahusiano ya mwanzo kati ya mwanamke na mwanaume kabla ya kufunga ndoa. Huwezi kuingia kwenye ndoa bila kupitia uchumba hivyo basi uchumba ni daraja la kupitia kuelekea kwenye ndoa. Hapa katika uchumba watu wawili hao kila mmoja asipokuwa wazi kuonyesha vilema au kilema chake ndio chanzo cha matatizo katika ndoa. Kipindi hiki cha uchumba kama wapenzi mnatakiwa kuwa wawazi, kila mmoja amjue mwenzake amchunguze na kumjua vema na pia kuwekeana misingi ya kuishi falsafa moja katika maisha yenu. Kama mtu ana ugonjwa wa kurithi ni vema amwambie mwenzake kama atakupenda akupende na kilema chako.

Ndoa ni makubaliano halali kati ya mwanaume na mwanamke kuishi kama mke na muwe. Ndoa ni makubaliano ya watu wawili kuishi kama mke na muwe bila kushurutishwa na mtu yeyote. Hapa siyo kipindi cha kuchunguzana bali hapa ni kuishi maisha ya ndoa na kuyafurahia.
Sasa tuangalie maadui wakuu katika uchumba au ndoa yako. 
Maadui wakuu katika ndoa yako ni kama ifuatavyo;
Maadui wa kwanza ni Nyinyi Wenyewe; usianze kumtafuta adui katika ndoa au uchumba wako kwanza jiulize na kujitafakari wewe mwenyewe kabla ya kuanza kumtafuta mchawi. Maisha ya ndoa au uchumba ni siri ya watu wawili sasa matatizo yanaanzia hapa kati ya wawili hawa kuanza kuanika hadharani mambo yao ya ndani baadaye mambo yanakwenda mrama huanza kulalamika na kumtafuta mchawi. Haitakiwi kueleza mambo yenu kwa watu hata

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA