HIVI UNAJUA KWANINI UNAENDA KUACHWA NA KUSEMA WANAUME WOTE NI MBWA


Kabla hujaita wanaume wote mbwa tulia Soma hii 

Chukua kikombe cha chai, kile kikubwa kabisa, pika chai yako nzuri, weka iliki, tangawizi, maziwa na kila kitu kizuri. Baad aya hapo inywe, unaona ilivyo tamu, ni tamu ee

 unatamani kuinywa kila siku. Basi sasa ongeza vijiko vitano katika kilekile kikombe, usiishie hapo, ongeza tangawizi vijiko kumi, hujaishia weka kiganja kizima cha iliki katika kile kikombe kimoja?

Unaona? Inafaa kunywa? Ni chai tena hapo au ni nini? Basi kama haifai kunywa hivi ndiyo wanawake wengi huachwa. Mwanzo wa mapenzi ni kama kile kikombe cha kwanza. Mnapigiana simu kwa kiwango, mnaongea kwa kiwango, mnaonana kwa kiwango, kulalamika nako ni kwa kiwango.

Lakini shida nhi pale mapenzi yanapokua matamu, wanawake huzidisha sukari wakidhani wanazidisha utamu kumbe wanaharibu. Anataka kukupigia simu kila dakika, akikuona online nataka uchart naye

 kutwa nzima, unakula umtumie meseji, unaingia kazini tutume, umetoka utume, yaani kila kitu kinazidi. Anataka kila siku muonane, ukimuambia niko bize basi anakasirika.

Anahisi kuwa uipo na mtu mwingine, anahisi kuwa unamdharau humthamini tena. Unaona dada mambo haya, basi unajikuta unazidisha kulalamika, unazidisha kuongea na mwisho mambo hufa. Kama mahusiano yameanza kupamba moto msome mpenzi wako, anataka nini, kuna ambao wanapenda chai iwe na sukari nyingi sana basi muweikee na kuna ambao hawatumii sukari kabisa usiweke.

Kunachokusukuma kufanya hivi nikwakua ukishapenda huamini kama kuna maisha mengine ziadi ya huyo mwanaume.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA