OMBA KWA KIPIMO MUME WAKO HANA KASHIMO KA KUCHIMBA PESA CHUMBANI


Hakuna sehemu akifika anafukua na kuchukua pesa, anatafuta tena kwa shida. Kwa maana hiyo kama una mwanaume angalau anakuhudumia na kujali ndugu zako basi hembu omba kwa kipimo na kama ndugu zako ni wale wa kuombaomba kila siku basi wewe kuwa ndiyo mtu wa kukataa. Kwamba kuna wanaume wengine wakiombwa pesa ukweni wanashindwa kusema hapana.

Kama una ndugu wana hiyo tabia ya kuombaomba, wapige marufuku kabla ya kukuharibia ndoa, mwanaume ambaye hawezi kukataa ana sifa moja, anatoa lakini anakasirika na kuwa na chuko za ndanindani, hawezi kusema hapana mbele za watu ila anasema hapana huko kwenye roho. Huyu ni mbaya kuliko yule ambaye anajua kusema hapana kwani anakaa na vitu vingi kwenye rohjo akipasuka anapasuka na kila kitu.

Kwanza si heshima ndugu zako kumuomba mume wako pesa moja kwa moja, wanapaswa kuongea na wewe ili angalau upime shida yao kama ni ya maana au ni yakuwakatalia, nyingine hasa ambazo si zalazima basi ukazinyamazia. Wakishaanza kumpigia Baba hiki, sehemu nina shida hii wanakuruka wewe basi jua kuwa mume wako anaweza kutoa lakini anaumia. Kumbuka kuwa mume wako anaweza kuonekana ana pesa lakini amini nikikuambia kuwa hata kama mume wako anajiweza ila ni lazima kuwa na mipango.

Kibaya zaidi nikuwa, ukishawazoesha ndugu zako kumuomba mume wako pesa moja kwa moja  basi kuna mambo mawili, kwanza siku akikataa au akiwa hana wanamchukia na kumuona mbaya, laki siku ukigombana naye basi hata kama yeye ndiyo mwenye kosa watakua upande wake, watakulazimisha kuvumilia si kwakua wanafurahia wewe kuteseka bali kwakua wanaogopa atasitisha huduma. Hivyo ni muhimu kuweka mipaka ya kuzoeana kati ya mume wako na ndugu zako!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA