KAMA ANAKUPA KILA KITU BASI JIFUNZE MAMBO HAYA MAGUMU HATA KUYAWAZA

Kama una mwanaume/mwanamke ambaye anakupa kila unapoomba basi jifunze kuweka akiba na kuwa makini usije kuwa mlemavu wa kipato. Nilazima ujifunze kutafuta cha kwako kwani katika maisha kuna mambo mawili, moja linaweza lisitokee na lapili ni lazima litokee. Jambo la kwanza ni kuchokwa, unapkua ni mtu wa kupokea tu na unatumia kama hakuna kesho basi jua kuna wakati huyo mtoaji atachoka kutoa.

Hapo ndiyo ataanza manyanyaso, atatafuta visababu vya kukufanya ujisikie vibaya ili tu kama una akili basi ujitambue kuwa unapasw akuacha kuombaomba na kuanza kutafuta. Hata kama kakukataza kutafuta anataka ujiongeze ulazimishie kwani anakua amekuchoka na kukuona mzigo. Hili ingawa hutokea kwa wengi lakini si lazima litokee, anaweza asikuhcoke na ukawa ombaomba wa kudumu.

Jambo la pili ambalo wengi hatatutaki hata kulizungumzia ni kifo, hili nilazima litokee, upende usipende, uwaze usiwaze, uongee usiongee. Sasa ukitangulia wewe unayemtegemea hakuna shida kwani sidhani kama kaburini utahitaji matumizi lakini kama akitangulia yeye basi jua kuwa utateseka sana kwani hujui namna ya kutafuta. Hivyo hembu kubaliana na ukweli, jifunze kutafuta na kutengeneza chako kabla haya mambo mawili hayajatokea.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA