HII KWA WANANDOA WOTE AU WACHUMBA


Kama mume wako anapitia wakati mgumu wa kikipato na ni mpambanaji muache bado awe mwanaume, narudia muache bado awe mwanaume. Si kila wakati mwanaume anafanikiwa, si kila wakati atakua sawa na si kila wakati mwanaume atakua na jibu la kila swali.
Kama wewe unafanya kazi na unacho hembu hudumia familia bila kinyongo wala kulalamika

Usiruhusu watu wa nnje kujua hali yenu ya ndani, si Mama yako, baba yako wala mashoga zako. Hata kama unaenda kuomba msaada huna haja ya kusema mume wangu haingizi chochote mimi ndiyo kila kitu ndani ya nyumba, chakula mimi, ada mimi, sijui hiki na kile Imimi. Wewe sema tu mimi na mwenzangu tumekwama, watu wazina watekuelewa. utasaidiwa bila kumdhalilisha mume wako,

Narudia acha kumtangaza mume wako kwa ndugu zako na mashoga zako kuwa hana kitu. Wakati mwingine mpe hata kama ni kidogo basi atoe mbele za watu. Msitiri kwa ndugu zako kwa kuseama mchango huu katoa flani na si kujifaharisha mbele yao kuwa wewe ndiyo umetoa na mume wako kaja kama mzigo. Fanya hivi kama mume wako ni mpambanaji.

Fanya hivi kama mume wako anaamka asubuhi anatoka kutafuta na harudi na kitu, fanya hivi kwakua wanaume watafutaji wana sifa mbili, kwanza hawachoki mpaka wapate, lakini wakipata hawasahau walipotoka. Ndiyo mwanaume mtafutaji mhangaikaji akipata hawezi kukusahau. Wanaume ambao wanasahau ni wale ambao hawana kazi. hawajishuhulishi, ukimpa mtaji anakula na hata kuhonga na hata hajali.

Huyu likinyokea zali akipata basi utaisoma namba, ila kama mwanaume wako ni mtafutaji, ni wale ambao wanahangaika mpaka wewe mwenyewe unamuonea huruma, kwamba ukimuangalia usoni unaona namna anavyoumia pindi wewe ukitoa pesa ya matumizi basi jua kuwa ni upepo tu mbaya umempitia, ataibuka. Muache awe mwanaume na msikilize zaidi kuliko ulivyokua unamsikiliza huko mwanzoni.
  MUNGU AWABARIKI SANA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA