IJUE TOFAUTI YA MWANAMKE ALIYE KWENYE NDOA NA AMBAYE HAJAOLEWA PINDI MAPENZI YANAPOMPA MAUMIVU💯

Kwanza fahamu kwamba maisha yanahitaji MAPENZI IMARA si kwa Mwanamke ama Mwanaume, Mapenzi yanabeba dhamana kubwa kuliko UNDUGU nyakati zile mtu anajihisi yupo katika MAPITO YA KI MAISHA.
Nirejee katika maana ya ANDIKO HILI :-
👉 MWANAMKE AMBAYE HAJAOLEWA ANAPOINGIA MIGOGORO KWENYE MAHUSIANO YAKE HUTAMANI MABADILIKO NA ASIPOYAONA HUOMBEA MAHUSIANO MAPYA 💯
Na hilo ndilo hubeba maana halisi ya UPENDO WA DHATI 💘 WA MWANAMKE kwa sababu kama Mahusiano yamekosa mvuto kuyalazimisha ni kujipa stress.
👉 MWANAMKE ALIYE KWENYE NDOA AONAPO NDOA YAKE HAIISHI MIGOGORO MARA ZOTE HUTAFUTA FARAJA ILI KUFUBAZA MAUMIVU YA NDOA YAKE 💯
Na hilo ndilo hudhoofisha FURAHA YA MWANAMKE kwa kujiona ni mhitaji wa FARAJA kuliko UPENDO na ndipo Mwanamke huyu huonyesha kutokuwa na UPENDO WA DHATI 💘 kama wanawake wengine, Maana anajihesabia ubinafsi kuliko hata maana halisi ya NDOA.
Huyo ndiye Mwanamke na tofauti yake pindi awapo Kwenye MAHUSIANO AMA NDOA na kila Mwanaume na ajue kukabiliana na Mwanamke wake kulingana na eneo alilopo, Kwamba :-
👉 KAMA NI MKEO BASI EPUKA KUPATA MSAIDIZI WA KUMJALI.
👉 KAMA NI MPENZI TU KUMBUKA AKICHOKA ATAONDOKA AKAPATE MWINGINE.
Itoshe kusema kwamba UISHI KWA AKILI 🧠 NA MWANAMKE 💃 WAKO hawa viumbe wanahitaji extra care Yaani usipoteze sekunde kumjaribu kama ANAKUPENDA.
#Elista_kasema_ila_sio_Sheria 🔨

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA