KAMA UNAFANYA MAMBO HAYA 3 BASI JUA UNACHEPUKA BILA KUCHEPUKA

(1) Umeolewa, umekutana na mwanaume huko mtaani. Amekutongoza au hajakuambia kuwa anakutaka, lakini anaonyesha dalili zote kuwa huyu mtu ananitaka kimapenzi. Huna Biashara yoyote kusema labda mtapeana madili, lakini hata kama unafanya Biashara ila unajua kabisa huyu mtu ananitaka kimapenzi ila anakuomba namba unampa.

Dada hapa unachepuka, kumpa namba mwanaume kama huyu ni kama ushamkubali. Hana haja ya kukutongoza tena ni kama ushakubali. Mwanaume kama huyu akituma meseji ataanza “Vipi mrembo…. Mpenzi mambo… nimekumiss… tunaweza kuonana darling….” Mume wako kama ana akili akiona meseji za namna hii ukimuambia ni rafiki tu anajua kuwa unachepuka.

(2) Umeolewa, unazunguka mtaani unakutana na X wako, mlishaachana muda na mshasahauliana, umke wa mtu kabisa lakini anakuomba namba yake ya simu na wewe unampanamba ya simu. X wako anakuomba namba ya simu kwakua wewe ni kiporo, anajua kuwa iopo siku atakutafuta na kukipasha.

Kwa maana hiyo kama mume wako akikuona unaongea naye, halafu umuambie alikua ni X wangu hatukuachana vibaya basi atajua tu wewe ushapashwa.

(3) Umeolewa, rafiki yako wakike anataka kutoka out, anakuambia anaenda kuonana na Bwana wake, labda ni mpenzi au naye kama yuko kwenye ndoa kama wewe ni mchepuko. Anakuambia huyo rafiki yake atakuja na rafiki yake, au hata hakuambii lakini unafika kule unakuta huyo rafiki yake amekuja na rafiki yake wakiume naye mnaanza maongezi kisha anakuomba namba unampa!

Huyu mwanaume anajua kuwa umke wa mtu lakini kakuomba namba kwakua anajua unajiuza. Anajua kuwa umeletwa kwake kwaajili yake ili akutongoze amalizane na wewe. Kama una akili utamuambia hapana, utatafuta sbabau za kumnyima namba basi. Ila ukimpa halafu mume wako akijua unaanza kusema nilimuona mara moja nilipelekwa na rafiki yangu mume wakoa tajua ni tabia yako na unajiuza.
 
(4) Kwa kifupi ni hivi! Kama umeolewa au uko kwenye mahusiano siriasi acha kutoa namba yako kijinga kijinga kwakua tu mtu kakuomba. Huna Biashara yoyote unatoa namba za nini? Sijui watakuja kukupa madili kwanini wasiwape dada zao, mpe mtu namba kama mliongea mambo ya maana, Biashara au mambo ya kazi, ila unaona kabisa anakutaka unampa namba, wanaume hatuna uvumilivu mlionao nyinyi.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA