KAMA UNA DADA WA NAMNA HII, TAFADHALI KUWA MAKINI NA NDOA YAKO

Kama una dada yako, ana miaka 30, hajaolewa, au aliolewa na kauchika, amezalishwa au hana mtoto, amekuja kuishi kwako, wewe una miaka 28-40, kwa maana kuwa umri wako ni bado kijana na mke wako ni umri wa miaka 30 mpaka 40, yaani wewe na mke wako ndoa yenu haijafikisha miaka 20, bado nyie ni vijana ndoa yenu bado changa, huyo dada yako amekuja kuishi kwako.

Ndugu yangu, mtafutie chumba, mpangishie akakae huko na kama hataki basi mfukuzie mbali, narudia, msaidie akiwa kwa mbali na kama ni lazima kukaa kwako si zaidi ya miezi mitatu. Kwani huyo dada yako atakuvunjia ndoa yako, narudia, ndoa yako kama haina maika 20 kuendelea basia cha kuishi na dada yako mtu mzima ambaye ndoa yake imemshinda au ana umri wa kuolewa na hanamtu.

Hao watu wana stress sana na kibaya zaidi wanaumia sana na kumuonea wivu mke wako, yaani unavyomjali mke wako, unavyomhudumia, unavyomnunulia zawadi, wanachanganyikiwa, wanaumia, wanalia kirohorohoro. Hakuna! Hakluna! Hakuna! Hakuna! Hakuna! Hakuna! Hakuna! Hakuna! Hakuna! Hakuna mwanamke wa miaka 30 ambaye anafurahia kukaa kwa Kaka yake.

Narudia hakuna mwanamke wa miaka 30 anafurahia kukaa kwa Kaka yake, kila mmoja anatamani kuwa kwa mume wake ni kwakua tu hana, hivyo ni lazima! Ni lazima! Nilazima! Nilazima kumuonea wivu mke wako, na usipokua makini taavunja ndoa yako! Yaani baada ya muda, utamuacha mke wako, ataondoka na yeye ataenda kuishi kwa Kaka yake au ataenda kuolewa na mwanaume mwingine na watoto wako watakua ni watoto wa kambo!

Najua Damu ni nzito kuliko maji lakini huwezi kutumia damu kupikia ugali! Kila mmoja ana umuhimu wake, msaidie Dada yako kwa mbali, narudia msaidie kwa mbali, ukimleta kwako jua anaua ndoa yako na mwisho atapata bwana wake, atakuacha na kwenda kuolewa! Hata kama dada yako anakupenda vipi, akipata mwanaume waake atakuacha, yuko kwako kwakua hana mwanaume, sasa mgande sijui akiolewa mtaenda wopte au itakuaje?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA