TAFUTA MTU WA HADHI YAKO ACHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO NA KUMLAZIMISHA KUFANIKIWA


Katika Mahusiano kuna hadhi, mwanamke, unapoingia kwenye mahusiano na mwanaume hakikisha kuwa huyo mwanaume ni wa hdadhi yako. Umemuangalia umemuona kuwa anakufaa na umekubaliana na alivyo. Sio una msongo wako wa mawazo, umechezewa huko kwenye mahusiano ya nyuma unaamua kumkubali Kaka wa watu.

Baada ya kumkubali, badala ya kumuacha awe na amani basi unaanza kumpigia kelele. “Nataka utafute bkazi, kwanini hauko siriasi na maisha, mbona wenzako wanajishughulisha… kwanini usinunue kiwanja, mara hiki mara kile!” Utamchosha tu mwanaume na yeye atakuchoka na kukuacha.

Si vibaya kumshauri mwanaume lakini kulazimishia ili awe na aina ya maisha unayotaka kwakua tu marafiki zao wanaume zao wana nyumba, wana magari, sijui wana nini ni kuchoshana na kueana STRESS. Kama unataka mwenye gari rtafuta, nyumba tafuta, Biashara tafuta, ana maisha mazuri tafuta.

Lakini unakuta kijana wawatu katoka zake chuo, hajapata kazi anahangaika na maisha unaanza kumlalamikia kwua hana “Future” kijana anaishi vizuri na ndugu zake karidhika unataka kumhamishia sijui nyumba ya bei ghali, sijui nini aisee inaboda badilika chagua mtu ambaye ni wa hadhi yako usitie watu stress!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA