TATIZO LAKO NI KUDHANI KUWA KILA WAKATI UNAKARIBIA KUACHWA KWAKUA TU HUJIAMINI.


Mapenzi yanapokua matamu au mambo yanapokua siriasi labda mwanaume kaja kujitambulisha kwenu, umebeba mimba yake na mna mipango ya ndoa. Mmefagnya kitu cha maendeleo kwa pamoja, kuna kawasiwasi flani kwamba kila kosa mpenzi wako analolifanya kama binadamu basi unaliona kama vile anataka kukuacha.

Kwa mfano, mlizoea wewe na mpenzi wako kila sikua subuhi anakupigia simu, mchana na jioni. Lakini ghafla hapigi simu asubuhi, au anapiga asubuhi ila mchana hapigi, au akikupigia simu basi hataki kuongea sana, anakua kama anaaga kisha anakuambia kachoka. Moja kwa moja bila kujua kuwa mambo yanabadilika basi unaamini kuwa kweli huyu mtu kabadilika na anataka kuniacha.

Unapaniki na kuanza kuuliza kila dakika unazidisha meseji na kupiga mara kwa mara. unaanza kukagua simu yake kila dakika ukitafuta ushahidi kuona kama anachepuka. Kama uko katika hali hii basi unapaswa kujua mambo haya matatu.

(1) Kuna wakati tu mtu anakua hana mood wa kuongea na wewe. Anakua bize, ana mambo yanamchanganya hivyo anahitaji muda wa kujitafakari. Kulazimishia kutaka awe sawa muongee ni kuzidi kuharibu.

(2) Ratiba zinabadilika, inawezekana kawa bize, kuna kitu anakifanya lakini hataki kukuambia. Sikwakua hakupendi bali kwakua si wakati sahihi.

(3) Ameenda kasi sana na anataka kujitafakari kama wewe ni mtu sahihi au la? Hapa si kama hakutaki, hapana lakini kama binadamu anapaswa kujiuliza mambo ni mazuri kweli lakini je hivi huyu ni mtu sahihi kwangu kweli? Usipompa muda ukizidisha kisirani basi unakuta ndiyo anaona kuwa hufai.

Katika mahusiano huu ndiyo wakati wa kujipa raha mwenyewe. Kupumua kidogo na kuacha kulazimishia kuongea naye. kama hujui namna ya kujipa raha mwenyewe hembu soma mapema kabisa Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha” yangu.

Usipokua na furaha kabla ya ndoa hata hiyo ndoa unaweza kuishia kuiona kwenye mitandao. Wanaume huoa ili kuwa na furaha na si kuoa ili kujitetea kila siku kama wapo polisi. Bei yake ni shilingi elfu kumi. Kupata kitabu unalipia kwa M-pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 Jina linakuja Iddi Makengo, sina namba nyingine zaidi ya hizo baada ya hapo Kitabu utatumiwa kwa njia ya Whatsapp, Email au Facebook.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA