Sababu 1 Kubwa Kwanini upo Kwenye MAHUSIANO Mazuri lakini Unaweza Kuachwa GHAFLA na Mwanaume!

Uko kwenye mahusiano mazuri, mnapendana na mwanaume wako, unaona kabisa huyu mtu ndiyo mtu sahihi, huna shida kabisa. Lakini ghafla unaona mambo yanabadilika anakua hapokei tena simu, anakua hataki kuongea tena na wewe kama zamani, anakua hajali tena. Unaanza kuwa na wasiwasi, unaanza kuhisi kama vile ana mtu mwingine, unakua na kisirani na mwisho unaachwa.

Sasa kama uko kwenye mahusiano mazuri ni lazima kujua ni kwanini mahusiano yanapokua mazuri sana yanaishia kuvunjika? Ukiachana na sababu nyingine nyingi ambazo zinakuja kichwani kwako kama vile ana mwanamke mwingine, labda flani kaingilia, labda umekua mbaya na labda mko mbali kuna sababu moja kubwa ambayo wanawake wengi hawaijui.

Kumfanya mwanaume wako kuwa kila kitu chako. Hii ni sifa ya wanawake wengi, wanapopenda na kuona kama wanapendwa basi husahau kila kitu na kutaka kufanya kila kitu na wanaume zao. Unataka mwanaume wako awe shoga yako, awe Mama yako, awe Bosi wako, muwe mnasali pamoja, mnatoka kila sehemu pamoja, akiwa online muwe mnachart pamoja na kila kitu mfanye pamoja.

Kuna wakati hii hali ni nzuri na mwanzo wa mahusiano hii ni tamu. Ila baada ya muda inaboa, inaboa kwakua wmanamke anataka akipiga simu ipokewe hapohapo, akichelewa labda kuna kitu alitaka kumuambia basi ananuna. Anataka aache urafiki na mwanamke flani akikataa basi ni kama kamdharau, anataka kila akiwa online ajibu meseji zake asipojibu basi ni alikua anachart na wanawake wengine.

Haiishii hapo, mwanamke ukishampenda mwanaume unataka afanikiwe ili “Akinioa aweze kuhudumia familia, tuwe na nyumba yetu, gari yetu…” kwasababu hii unamsikuma mwanaume wako kufanikiwa. Akitumia pesa vibaya basi unaanza kulalamika, ukimshauri kitu labda kununua kiwanja akanunua gari basi unaksirika na kuona kama hana mango ya kimaisha.

Dada mwanaume anajua unampenda na vitu unavyovifanya si vibaya lakini vinachosha. Unakua kama ushakua mke wake kabisa, unakua kama unampangia, unambana sana humpi pumzi hivyo kumfanya mwanaume aliyekua anakupenda akuchukie. Wanaume wengi wakishafikia katika hali hii hutaka kupumua, hupunguza mawasiliano, wanakua hawatamani tena kuongea na wapenzi wao.

Sasa wewe mwanamke mwanaume wako akipunguza mawasiliano unazidi kuchanganyikiwa.

(1) Unampigia simu hajapokea basi unamtumia meseji zaidi ya 100. Unakumbuka mambo uliyoandika, hajakujibum lakini bado unaandika, unahisi umeachwa, kuna kakitu flani kanakuingia kama vile usipotuma meseji ya pili hatajua kama unaonyesha msisitizo.

(2) Unaanza kukumbushia mambo ya zamani mambo ambayo alikufanyia. Kuna mambo alikosea, ukamsamehe lakini baada ya kuhusi kabadilika basi ni meseji za kukumbushia, kipindi kile hivi, kipindi kile vile! Unalalamika sana mpaka inaboa na bado hakujibu.

(3) Unakumbushia mambo uliyomfanyia. Hapa ndiyo kazi, ulimkuta hana kazi ukamsaidia kupata unakumbushia, ulishamkopesha pesa basi unamkumbushia, ulimsaidia kitu flani unamkumbushia na kuona kama hana fadhila.

(4) Unaanza kutafuta ndugu zake. Hajawahi kukutambulisha kwa ndugu zake lakini utawatafuta mpaka kuwapata, labda alikiutambulisha utaenda kuwaambia kuwa kabadilika. Lakini huishii hapo, unawamabia na mambo mengine, namna alivyobadilika, machafu yake, unawasumbua na kuwaomba kuongea naye, nao wanakupuuza unaona kama vile lao moja mnagombana.

(5) Unaanza kumuambia tuachane. Kwakua kakukalia kimya mwezi mmoja au hata wiki tu unahisi kakuacha. Basi ili kumtishia kupima kama anakupenda au la unamuambia tuachane, wakati mwingine unamuambia ili tu asianze yeye kukuacha basi unamuambia tuachane na akikaa kimya unazidi kuchanganyikiwa.

NINI CHA KUFANYA HAPA; Najua umepaniki na kuchanganyikiwa kabisa, lakini hembu punguza kasi. Kuna wanaume wanapenda kugandwa lakini kuna wengine tena ndiyo wengi wanataka mwanamke kuwa na maisha yake. Hivyio mwanaume akianza kupunguza ukaribu hembu acha kupaniki, hujaachwa bado, lakini hata akikuambia mpeane nafasi bado hujaachwa.

Wakati mwingine anataka tu kujitafakari hivyo kua mpole, usimgande sana, acha kuongea na rafiki zake au ndugu zake unaharibu zaidi. jipe muda wa kjujipa furaha yako mwenyewe mambo yatajipa ila ukizidisha meseji na simu utaharibu. Kama hujui namna ya kujipa furaha yaki mwenyewe soma Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” Sehemu ya Nne.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA