MAPENZI YANAYOTESA NA KULIZA WENGI YA VITU SI YA UTU.

Leo ukiona mapenzi yenu hayana ushirikiano,ya kupinduka pinduka,mnapata asubuhi jioni mnanuniana ni wazi kabisa kuna mmoja ana mapenzi ya maslahi yake binafsi.
Mapenzi binafsi kwa maana akuangalii wewe bali anatazama kile kilichopo kwako ili kumnufaishe yeye,anajiangalia yeye kwa faida zake yeye.

Mapenzi yote yenye amani kwa asilimia 75 ni mapenzi ya kweli.
Wanatofautiana kwa mambo ya kibinadamu na ndio mapungufu yenyewe.
Kuna mahusiano watu wanayaishi asilimia 75 zote ni za kashi kashi,ugomvi nyakati zote na wapo awaachani,kesi kila mara kwa wazee wa kanisa,kwa mashekhe hata kwa wazazi.

Ukiona,mkiona ndani ya nyumba amani ndogo,furaha ndogo,faraja hakuna ni wazi hakuna upendo.
Inafika hatua mmoja ikitokea ametembea safari ya mbali hata akae mwaka mwenzie hana habari nae,ashtuki hata kumuuliza lini anarudi,kipimo cha wazi hakuna upendo wa kweli. 

Upendo wa kweli ni wa mtu na mtu sio upendo wa mtu na vitu.
Ukipendwa kweli uangaiki kudai kitu wala kuomba kitu.
Ukipendwa na mtu utapewa kila hitaji la upendo upaswi kudai,ni automatical inakuja tu.

Mtu anaekupenda anafanya reseach ni unapenda,nini upendi,furaha yako nini,amani yako ni then anakutendea yale unayoyataka  na sio kukukadilia,sio kwa kubahatisha.

Ukiona unatendwa na kuteswa mara kwa mara ujapendwa,upendwi kwa utu wako uenda unapendwa kwa vitu vyako,ila yupo mtu anapewa kila kitu na huyo huyo anaekutenda.
Chukua hatua.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA