Mtu anavyokufanya ujione kama HAKUHITAJI basi usiondoke kwake ili ajihisi hatia au asikitike maana hilo halitaweza kutokea.


Ondoka katika maisha yake kwa sababu kubwa moja tu, kwamba hujaona sababu yeyote ya kuendelea kuwa na yeye au inayokufanya upiganie mahusiano hayo.

Inafika kipindi mtu lazima uwe na ujasiri dhidi ya hatima ya maisha yako kwa sababu jambo ambalo umeandikiwa kuwa nalo, litakuwepo kama hukuandikiwa haliwezi kudumu.

Ndio, Mahusiano yanafaa kupiganiwa lakini sio wewe peke yako unaetakiwa kupigania. Muda mwingine mtu unayempigania na yeye lazima azione jitihada zako na kuzithamini walau hata kidogo.

Kama hana muda huo, itoshe kutambua kwamba unachompa ni zaidi ya anachostahili.

Kuwa sehemu ambayo moyo wako unahisi unathaminiwa, jitihada zako zinaenziwa na mchango wako unatambulika. Sio sehemu ambapo unavumilia.

"Don't try to force anything. Let life be a deep let-go .
God opens millions of flowers every day without forcing their buds."

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA