UKIONA MCHEPUKO WA MUME WAKO UNAKUJA NA STORI HIZI JUA USHAACHWA


Habari za majukumu kaka, mchepuko wa mume wangu umekuwa ukinitafuta na kunitumia sms kibao na kunieleza mambo mabaya kuhusu mume wangu, sijajua ni kwa nini ameamua kunitafuta baada ya kuwa na mahusiano na mume wangu kwa takribani miaka mitano, anakuja ananiambia eti kazaa na mume wangu, sijui mume wangu ameoa mwanamke mwingine, nimfanyeje huyu dada? Mume wangu sijawahi kumuuliza chochote.

JIBU LANGU; Dada kama wewe ni mtu wa Mungu basi huu ndiyo wakati wa kutoa sadaka ya shukurani. Ukiona mchepuko wa mume wako unakutafuta na kujifanya una raha basi jua kuwa ushabuma. Narudai, mchepuko wenye raha hauna haja ya kukutafuta, hauna haja ya kukuambia mambo yake, yaani utakula kimya kimya hata inzi hawatajua.

Lakini kamchepuko kakishaanza sijui mimi ndiyo napendwa, sijui wewe kaa uzae mimi nakula maisha, sijui mume wetu hivi basi jua kuwa mambo huko yashaanza kuchemka. Yaani ni kama maharage, yanarukaruka tu yakiiva, endelea na maisha yako baada ya muda atatulia.

Dada kama wewe ni mstaarabu akikutafuta muambie tu “Umetumia viungo vyako huna haja ya kunipa taarifa” kisha achana naye, akipiga simu pokea, weka chini nenda kaoshe vyombo. Akituma meseji hata usifungue. Kuzaa kitu gani anakuringishia mtoto wakati hata sisi mizi wanzaa lakini hawaringi tunawakanyafa nini? Askikuambia kanizalisha muambie akazane azae wapili utamsaidia kumpa jina!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA