UNAINGIA KWENYE MAHUSIANO? BASI KUWA MAKINI NA AINA HIZI TATU ZA WANAUME!


(1) Mwanaume aliyetoka kuumizwa kwa kuachwa wakati anapenda; Umekutana naye, ndiyo katoka kuachwa, mwanamke aliyekua anapendana naye kamuacha kaenda kuolewa na mwanaume mwingine, ana mimba ya mwanaume mwingine au kamuacha kwa dhatrau. Rafiki zake au ndugu wanakumbia kuwa flani alimuumiza sana, yeye mwenyewe haipiti siku hajamzungumzia, unakuta bado ana vitu vya huyo mwanamke na ukitaka kuviondoa ni ugomvi.

Wakati mwingine bado anamtafuta au mwanamke akimtafuta anawasiliana naye. Dada yangu kuwa makini sana na huyu mtu, mara nyingi mahusiano yake ya kwanza baada ya kuachwa kwa kudhalilishwa akaumizwa sana ni ya kupunguzia maumivu, ni mahusiano ya dawa, anayatumia kujitibu, huyu kuna uwezekano wa mambo mawili kutokea. Kwanza akishapona kugundua kuwa alikua na wewe kimakosa akakuacha, pili asipone kabisa, hata akakuoa lakini asimsahau huyo mwanamke.

Yaani hata akipigiwa simu usiku anaweza kwenda, yaani utahangaika kila kitu lakini hamsahau. Dada yangu mwanaume aliyeachwa akaumia unamuona tu, kama hataki kuondoa vitu vya huyo mwanamke wake, kama akimzungumzia anamzungumzia kwa hasira, anatukana na kusema sitapenda tena, haamini wanawake, kama ndugu wanakusisitizia sana uwe naye, kila siku wanasema aliumizwa wanakutaka wewe basi huyo mwanaume kuwa makini naye, sikuambii umuache ni maamuzi yako ila una akili zako kuwa makini naye.

(2) Mwanaume ambaye umemzidi kila kitu; Umemzidi elimu, umemzidi kipato, umemzidi hata akili tu za maisha. Huyu si tatizo sana ila kama hajiamini na vitu vyako basi ni tatizo. Mkigombana kidogo anaanza ni kwakua umesoma, nikwakua una pesa, ni kwakua hivi na vile. Aisee kuwa makini kwani hajiamini na anahisi kuwa unamnyanyasa kwakua umemzidi, yaani huyu hata ukimlamba miguu basi atalalamika unamlamba kwa nguvu kwakua umesoma.

Kama ni mahusiano ya kawaida na hujampenda sana unaweza kumuambia kwa heri kwakua hawa bwana siku wakipata kwakua walikua wanaamini unawadharau basi watataka kuonyesha makucha yao na kukudharau pia. Kuwa makini, kama unabaki na mwanaume wa namna hii basi acha kulisha kutokujiamini kwake, kuwa wewe, acha kumnyenyekea na kujaribu kujishusha sana ili tu mlingane, hapana, hamalingana zaidi utamvimbisha kichwa ili azidi kukunyanyasa.

Eti uache kazi ili arihdike hataridhhika, ujenge nyumba uandike jina lake ilia jihisi mwanaume hatajihisi, ufungue bishara umpe ili ajihisi mwanaume akifanikiwa atatumia kuhonga, eti uache kuwa namarafiki wasomi kwakua yeye hajasoma, bado atakasirishwa na wafanyakazi wenzako. Kwakifupi iko hivi huwezi kumridhisha mtu ambaye  hajiamini na kila dakika anahisi kama anaonewa, cha kufanya ni wewe kuishi maiha yako, ushmdharau lakini usijishushe sana mpaka kufikia hadhi ya takataka, akiwa juu hatakukumbuka!

(3) Mwanaume ambaye kila kitu ni Mama, Mama, ndugu ndugu; Hawa ni wale wanaume ambao ukiwa nao unafikiri unatembea na Mama zao au dada zake,.yaani kila kitu ni Mama kasema, Mama hivi, niliongea na dada niliongea hivi! Hawa ni kama watoto ambao hawajavunja ungo, hawana siri kila kitu ni lazima waende wakaseme. Yaani ukute ana na vihela vihela, Mama yake ndiyo anamuamulia kila kitu ndiyo utaisoma namba maana kila mkipanga kitu itakua ni Mama.

Najua hutamuacha hivyo cha kufanya ni wewe kuwa na misimamo yako, usiyumbishwa kwakue Mama yake kasema. Kubaliana na baadhi ya mambo lakini weka mipaka, chora mstari chini na sema kuwa nitafanya kila kitu lakini hiki hapana, hiki ndiyo, hiki poa. Ukiwa na mipaka si yeye wala ndugu zake wanaweza kukusumbua. Kama ndiyo uko kwenye mahusiano kuwa makini na vitu kama kuacha kazi, kufungua biahsara ya pamoja wala kujega pamoja, ndugu zake wakijua kwanza watadhani ni vyao.

Pili watataka kuviawala na tatu ukileta ubishi basi hata ndoa utaisikia kwa Mangi. Ukiingia kwenye ndoa na mtu wa namna hii jua kuwa, kila kitu atashirikisha ndugu zake, kwa maana hiyo vitu vya maendeleo hasa vyakudumu hakikisha vina na majina yako. Ukicheza ukamuachia akaandika majina yake basi ni rahisi kuvibadilisha kwenda kwa ndugu zake kwani ndiyo wanamuendesha. Kwa ushauri zaidi soma kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu’ na ukikwama nipigie baada ya kununua kitabu!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA