MWANAUME WAKO AMEPUNGUZA MAWASILIANO BAADA YA KUPATA KAZI? SOMA HAPA KABLA HUJAHARIBU MAMBO!


Mawasiliano ya mwanaume akiwa hana kazi ni tofauti kabisa na pale anapokua na kazi. Kwa wanawake wengi hudhani kama Mwanaume kabadilika, labda amepata mtu mwingine na hivyo kuanza kulalamika, kununa kila saa kwakua tu mtu aliyekua akikupigia simu mara nne kwa siku basi hupiga mara moja au kutokupigia kabisa.

Ni kweli kama Mwanaume anaweza kukaa wiki hakutafuti unapaswa kushtuka lakini suala la kukaa kutwa nzima bila kukutafuta au kukupigia mara moja kwa siku halipaswi kukuumiza kichwa sana. Alipokua hana kazi alikua na muda pamoja na Mood ya kukutafuta, ila kazi mbali ya kumfanya kuwa bize basi huleta stress, kuna mambo haya ya kuyajua.

(1) Kabla ya kuwa na kazi alikua hana mambo mengi ya kuwaza zaidi yako hivyo alikua akikutafuta mara kwa mara, ila baada ya kazi anakua bize, ana mambo mengi ya kuwaza, ana deadline nyingi, ana kupambana na bosi hivyo anakuatafuta akiwa na muda tu.

(2) Kabla ya kuwa na kazi alikua anakutafuta kwakua kaboreka. Hapa mnielewe, si kila wakati akikutafuta alikua anakumiss, hapana, wakati mwingine alikua bored tu hivyo hana mtu wa kuongea naye anaona akutafute umpotezee muda. Lakini anapokua na ikazi kwanza kazi zinambana lakini huko kuna marafiki wapya hivyo haboreki kihivyo ndiyo maana hakutafuti sana.

(3) Hakua na mawazo sana kipindi hicho, hakua na watu wengi wa kumchanganya. Kabla ya kazi alikua peke yake, hana bosi wa kumtukana, hana wateja wa kumpigia kelele. Lakini baada ya kupata kazi akili wakati mwingine inakua haiku sawa tu, mara katukanana na bosi, kagombana na mfanyakazi mwenzake, kabishana na mtaja, hata akikupigia simu mtaishia kugombana tu hivyo anaona asubiri jioni kichwa kikitulia ndiyo akutafute.

(4) Alikua anaogopa kukupoteza hivyo anakuchunga zaidi. Mwanaume akiwa hana kazi hana pesa, kila dakika anawaza kuachwa tu, kwa maana hiyo anakua na wivu zaidi anajua nisipomtafuita ataniacha. Lakini akiwa na kazi kakujiamini kanakuja, anakua haogopi tena kuachwa na hivyo hana haja ya kukutafuta sana.

(5) Mwisho ni hivi, mambo hayawezi kuwa kama zamani, mtu ambaye yuko bize na kazi hawezi kuchart kutwa nzima kwa maana hiyo badala ya kumuwekea kisirani kulalamika kua hakujali jua kuwa maisha yamebadilika ashakua mtu mzima kuna mambo nayo ni lazima kubadilika.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA