*💍-AINA 10 ZA WANAUME KERO KWA WAKE ZAO.


*💘-Aina Kumi Za Waume Ambao Wake Zao Wanakereka Kuwa Nao Illa Wanavumilia Tu Kuishi Nao.*

*💘-Kila ndoa ina changamoto zake. Na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wanandoa kuvumiliana katika changamoto hizo.* 

*💘-Kuna changamoto za kiMungu ambazo wanandoa hawawezi kuziepuka lakini kuna zile za kiwanaadamu ambazo nyingi ni za kimakusudi na mtu huamua tu kuwa ivyo.* 

*💘-Katika kuangalia ndoa leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao.*

*1. "KING HUSBAND":-*
*💘-Hawa ni wanao jiona kama wafalme.*

*💘Hii ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutuma tuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kufanya kila kitu.* *Wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo.*

*💘-Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini. Wote kimya hakuna hata kuongea.*

*2. "BACHELOR HUSBAND".*
*💘-Hawa ni wanaume wanaojihisi bado hawajaoa.*

*💘-Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote.* *Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa. Hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui. Mke anaweza kushtukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha.*

*💘-Hajali kama ana mke na muda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.*

*3. "ACIDIC HUSBAND".*
*💘-Hawa ni wanaume wenye gubu.*

*💘-Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya msingi. Mambo hayaishi. Kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo.*

*💘-Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi ndani ya nyumba.*

*💘- Mke akiomba hela ya chakula ni shida. Ni kununa kutwa nzima.*

*💘-Wana hasira na ni rahisi kumpiga mke.*

*4. "GENERAL HUSBAND".*
*💘-Huyu ni mume wa kila mtu.*

*💘-Pia wanajulikana kama "Community Husbands.*

*💘-Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wa kike wa mke na wa kwao kuliko wanavyowajali wake zao.*

*💘-Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa.*

*💘-Wana marafiki wengi wa kike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma "X" wao. Wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.*

*5. "DRY HUSBAND".*
*💘-Hawa ni wanaume mabakhili. Wachoyo sana mpaka kwa wandani wao.*

*💘-Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani.*

*💘-Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke. Mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi.*

*💘-Kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kishamba.*

*💘-Yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wake zao.*

*6. "PANADOL HUSBAND".*
*💘-Hawa ni wanaume wanaopenda kutumia wake zao.*

*💘-Pia wanajulikana kama "Paracetamol Husband".*

*💘-Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida. Wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali.*

*💘-Wanapomhitaji mke, wanapotaka mke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vijizawadi.*

*💘-Wanajua udhaifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata hawajali tena.*

*7. "BABY HUSBAND".*
*💘 ni wanaume ambao hawataki kukua.*

*💘-Bado wana tabia za kitoto. Hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao.*

*💘-Mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwe. Na mke akifanya kosa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake. "Mbona flani alifanya hivi? Flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo".*

*💘-Kwa kifupi, hawawezi kufanya maamuzi na mkewe.*

*💘-Ndugu zake, haswa mama yake, anakuwa kama sehemu ya ndoa yake.*

*8. "VISITING HUSBAND".*
*💘-Huyu naye ni mume mtalii.*

*💘-Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile. Mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake.*

*💘-Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga. Na hana sababu za msingi za kuchelewa. Hata mwisho wa wiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke.* 

*💘-Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake. Kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nje tu lakini si kukaa na mke au watoto.*

*9. "STALKING HUSBAND".*
*💘-Hawa ni wanaume wanaofuatilia kila kitu.*

*💘-Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu. Huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hakupi pumzi.*

*💘-Mke akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani.*

*💘-Huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti.*

*💘-Ana wasiwasi na kila anayeongea na mkewe huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa kike wa mkewe pia huhisi wanamgawadia.*

*💘-Kwa kifupi, hampi pumzi mwanamke.*

*10. "MISERLY HUSBAND".*
*-Huyu ni mwanamume mchoyo.*

*💘-Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbakhili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti za mwisho. Anafuatilia mpaka mambo ya jikoni.*

*💘-Sukari ikiisha na anataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao. Huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela.*

*💘-Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.*

*👉🏾Hizo ni baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao.* 

*💘-Kama mwanamume upo hivyo jua mke wako hafurahii anavumilia tu.*

*💘-Ndoa ni furaha, amua kubadilika usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha.*

*💘-Kama ni mume, jiulize uko namba ngapi hapo na ujirekebishe.*

*💘 mke pia mezea namba ya mumeo jamani usimuumbue.*

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA