UNATAKA KUFANIKIWA HEMBU JIONGEZE INAKUONGEZEA THAMANI


Mwaka jana nilianza Biashara ya chakula cha mifugo, nilikua napata hasara sana niliamua kununua Kitabu chako ili kuongea na wewe kwani hii sehemu niliyopo kuna wafugaji wengi lakini nilishangaa kuona kama siuzi kitu. Nilipokupigia ulinishauri mambo mawili, jambo la kwanza uliniambia nimfukuze kazi mdogo wangu na jambo la pili uliniambie nianze kuwatafutia wateja wangu wateja wa bidhaa zao ili walazimike kununua kwangu.

Nakumbuka uliniambia kuwa mdogo wangu anajifanya msomi na analeta digrii yake kwenye chakula cha kuku hivyo kwa namna nilivyokuelezea nikuwa ana ringa kwakua anaamini kuwa mimi nina pesa nyingi hivyo haina shida hata akiwadharau wafugaji ambao wengi anawaona kama vile si wasomi na wana maisha magumu. Uliniambi nitafute mtu ambaye naweza kumfukuza kazi mtu ambaye ataihehsimu kazi yake na si mtu ambaye anaifanyafanya kwakua tu hana kazi anasubiri hadhi yake.

Ukaniambia kitu kingine nikuwa, sehemu nilipo wauzaji ni wengi hivyo ili kuwalazimisha watu kununua kwangu nilazima mimi kuwapa kitu ambacho huko kwingine hawawezi kukipata. Ukaniambia wafufaji wanazalisha kuku wa nyama na Mayai, hii ikimaanisha kuwa wanahitaji wateja wa kuvinunua hivyo. Ukaniambia kuwa niwe natafuta tenda za watu wanaonunua kwa wingi na hata wanunuzi wadogo wadogo. Ukaniambia kwamfano kama nikipata mtu anahitaji kuku wa sherehe basi nampigia mteja wangu na kumpa hilo dili.

Nikipata mtu anahitaji mayai nampa dili hilo mteja wangu wa chakula cha kuku wa mayai. Ukaniambia nikiwapa hivyo inamaana nao watalazimika kujipendekeza kwangu kwakununua kwangu ili madili yakitokea wayapate kwani hata wao hali ni tete wateja ni shida hivyo tusaidiane. Kaka nashukuru nimemuondoa mdogo wangu na nimeanza kutafuta madili sasa hivi nina namba za wateja wa chakula na namba za wateja wa mayai na kuku.

Kaka umenisaidia sana kwani nina wateja ambao hata kama chakula kimeisha wananipigia nikachukue kiwandani niwapelekee kwakua tu na mimi nikisikia dili la kuku au mayai nawatafuta. Uliniambia niwe na ukaribu na watu wanaopika kwenye mashughuli kaka mimi nimtu wakujichanganya umbea wote mjini ninao na unanisaidia kupata tendatenda na sasa hata kwenye maduka nawaunganisha wateja wangu wanapeleka mayai, kaka nashukuru ushauri wako umenifungua sana na kuniwezesha kufanya Biashara vizuri.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA