KANUNI NAMBA 1 UNAYOPASWA KUIJUA KAMA SINGLE MOTHER UNATAMANI KUWA NA FURAHA

Kama wewe ni “Single Mother” unatakiwa kujua kuwa, mwanaume pekee ambaye unapaswa kumleta kwako na kulala ni mume wako tu. Tena hata mume mwenyewe ni umeolewa na wewe kwenda kwake na si aje kwako. Huna haki tena ya kuanzisha mahusiano kama msichana, unapaswa kuanzisha mahusiano kama Mama hivyo wanao ndiyo wanapaswa kuwa kipaumbele chako cha kwanza. Kabla hujapaniki hembu nikupe sababu hizi tatu.

(1) Umekutana na mwanaume, umependana, mmeanza mahusiano, anakuja kwako kila siku au mara kwa mara, analala kwako, watoto wanamzoea na wanajiongeza kuwa huyu ni Baba? Baada ya muda mnakorofishana, mnaachana, ghafla watoto hawamuoni tena, lakini wewe ni binadamu, unatafuta mwingine naye unamleta kwako, mnakorofishana mnaachana hivi unafikiri watoto watakuelewaje? Hata hawatajali kwanini mmeachana bali watajua kuwa Mama yao ni Malaya na niamini nikikuambia kuwa hawatakuheshimu tena!

(2) Umepata mwanaume, unamleta kwako, umemtambulisha kwa wanao, jamaa anapenda watoto sana, yaani kawa zaidi ya Baba yao. Kwakua wanao hawajawahi ishi na Baba wanampenda na kufurahia kampani ya Baba, wengine unakuta alimkuta mtoto akiwa mchanga, anamlea mpaka amekua mkubwa. Ghafla watoto wamempenda mnagombana, mnaachana sasa kila siku watoto wanauliza Baba yuko wapi, unaumia wewe na kuwaumiza watoto pia.

(3) Najua ushaanza kuwaza mbona Kaka iddi anawaza kuachana sana, lakini ukweli nikuwa uwaze usiwaze kupo. Kama single mother ni lazima kuwafikiria wanao namna ambavyo wataathirika na wanaume wako, kanuni ya kwanza mwanaume asilale kwako, ya pili mtambulishe kama anko. Kanuni ya tatu awapende wanao lakini ukaribu wao uwe wa mtoto na anko na si mtoto na Baba yake, akikuoa sawa ila kabla, usijidanganye kuwa hakuna kuachana.

Kila mwanamke anapopenda sana hawazi kuachana lakini ukweli nikuwa kupo ndiyo maana hata Baba yao inawezekana mliachana. Najua wakati mwingine ni ngumu, lakini hmbu fikiria, wanao hawakumpata Baba yao, hawaishi naye, sasa hivi kumekuja mwingine, wanamzoea kidogo naye anaondoka. Mnapendana sawa lakini haimaanishi ndoa si lazima, mwanaume akikuacha akuache wewe lakini asiumize na wanao.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA