UNAMTAMBUAJE RAFIKI MWENYE DALILI ZA KUJA KUWA ADUI??

TEE
UNAMTAMBUAJE RAFIKI MWENYE DALILI ZA KUJA KUWA ADUI
Rafiki anaweza kuja kuwa adui au msaliti kwenye mambo mengi yakiwemo
• Kwenye mapenzi
• Kwenye biashara
• Kwenye kupata nafasi kazini
• Kwenye mahusiano na marafiki zenu
• Kwenye mikataba au tenda
Dalili/Mazingira
• Unasikia au unagundua anakusema vibaya kwa wengine, tofauti na akiwa na wewe
• Unahisi au unagundua anakupinga au kukuonea wivu kwenye mambo fulani
• Unahisi au kugundua nia yake ya kutamani kupata zaidi yako
• Unahisi au kugundua kuwa ushauri anaokupa sio wa kukusaidia bali wa kukukwamisha huko mbeleni
Unafanyaje?
• Usimwamini sana mtu wa namna hii
• Usijiachilie na kuwa wazi sana kwa mtu huyu
• Pima ushauri wake na ikiwezekana uliza mtu mwingine pia
Bora nusu shari kuliko shari kamili
Tags

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top