WANAWAKE SI KAMA WANAUME AKIKUPENDA HAWEZI KUKAA BILA KUWASILIANA NAWE

 WANAWAKE SI KAMA WANAUME AKIKUPENDA HAWEZI KUKAA BILA KUWASILIANA NAWE

by 

IDDI MAKENGO


IDDI MAKENGO; Natamani nikudanganye lakini ukweli nikuwa, huyo mwanamke si wakwako, nina uhakika ana mtu wake, kuna mambo mawili. Kwanza inawezekana ana mwanaume wake ambaye anampenda lakini haeleweki hivyo amekushikilia wewe kama kitu cha daharura, pili kuna mwanaume wake anampenda sana lakini hana pesa au anazo ila hatoi, ila kwa ulivyonieleza huyo si mwanamke wako.

MTEJA; Lakini ana mimba yangu na mimi nahudumia kwa kila kitu?
IDDI MAKENGO; Hapana, mimba si yakwako, huyo mwanamke ana malengo ya mbali, hawezi kuzaa na wewe kwakua hana malengo na wewe. Mwanamke anayekupenda hawezi kukaa mwezi bila kukupigia simu, mwanamke anayekupenda hakutafuti pale tu akiomba pesa, mwanamke anayekupenda hakufichifichi kama shanga za motoni. Mwanamke anayekupenda huliilii na kuomba kujitambulisha kwao kama vile unaomba uhai, narudia ana mtu wake.

Najua watu kama wewe ni ngumu kuamini, mkishapenda mnachanganyikiwa, ila fanya kitu kimoja. Kesho mtafute, muambie kuwa umepata matatizo kazini, muambie kuwa sasa hivi huna pesa hivyo akuvumilie kidogo. Acha kumpa pesa kisha nipigie baada ya mwezi mmoja niambie nini kimetokea.

MREJESHO; Nilifanya kama ulivyoniambia, nikamuambia kuwa nina matatizo kazini, nikamuambia kuwa anivumilie kwakua sina pesa. Mwanzo alikubali na kusema sawa, ial siku mbili baadaye aliniomba pesa, akaniambia anaumwa, nikamuambia sina hata pesa ya kula atumie akiba yake. Alichonijibu nikuwa, kama sina pesa ya kuhudumia mtoto basi atoe mimba, nikamuambia sitaki atoe lakini pesa sina.

Alikaa kama wiki mbili hivi akaniomba tena pesa, nikamuambia sina, akaniambia kuwa kama siwezi kumhudumia basi ni bora hiyo mimba ampe mwanaume mwingine na mimihanitaki tena niendelee na maisha yangu. mpaka sasa hivi nikimtafuta kaninunia, nikitafuta rafiki zake wananiambia kuwa nimemuumiza ndiyo maana kaamua kuninunia, sijui nifanye nini?

IDDI MAKENGO; Hiyo mimba haikuwahi kuwa ya kwako kama ambavyo huyo mwanamke hakuwahi kuwa wakwako. Mwanamke hawezi kusema mimba nampa mtu mwingine kama hakuwahi kuwa na mahusiano naye, alikua mtu wake ndiyo maana kampelekea.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA