WIVU UKIZIDI MWANAMKE ANAKUONA KAMA HUJIAMINI


Hakuna wanaume warahisi kuwachukulia wapenzi/wake wapenzi wao kama wanaume wenye wivu wa kupindukia. Kama wewe ni mwanaume ambaye, ukikutana na mtu kasimama na mpenzi/mke wako hata kabla ya kuuliza ni nani ushapaniki na kununua, kama wewe ni yule ambaye, kila siku unakagua simu ya mpenzi wako, ukaangalia namba ukiona ya kiume unapiga na kuuliza wewe nani?

Kama wewe ni yule, umekaa sehemu mtu akapita tu na kumsalimia mpenzi wako basi unanuna na kuanza kuvimbisha mashavu, kugombana kabisa mpaka unaanza kutukana basi mpenzi wako akikutana na baharia ni dakika mbili. Ni rahisi kumtongoza mwanamke wa namna hii kwasababu kuu mbili. Kwanza nikwakua hana furaha yale mambo anayofanyiwa yanamkera na kumnyima amani hafurahii kuwa na wewe kwakua kila siku mnagombana.

Kuna mara zaidi ya 100 alishafikiria kukuacha lakini akiwaza muda mliotumia, akiwaza watoto labda na shida ya kupata mwanaume mwingine anajiambia ngoja nivumilie atabadilika. Kwa maana hiyo akipata mtu mwingine anasema afadhali nipumue na hiki kisirani. Lakini jambo la pili, kumchunga chunga mwanamke ni ishara kuwa hujiamini, kwamba unaogopa kuachwa, huwezi kuishi bila yeye, unaogopa wanaume wenzako na ni ishara kuwa unajidharau.

Sasa kiasilia wanawake hawapendi wanaume wasiojiamini, yaani wanaketeka mpaka basi. Unajua wanawake wanaamini kuwa kutokujiamini ni tabia za kike, ndiyo maana wao wanahangaika na simu, wanahangaika kupigia wanawake wengine simu na kuwaambia “Achana na mume wangu!” wanalia, wanafuatilia, yaani sasa wakimuona mwanaume wanakua hivyo wanaona kama wako na mwanamke, wanakereka, yaani wanaboreka kama kumuona mwanaume analia au analalamikia tumbo la uzazi!

Wanaona ni mambo ya kike, hivyo mwanamke kama huyu akikutana na Baharia anayejiamini hata kama hana pesa akimtongoza hachomoi kwani ni kama anajihisi kutongozwa na mwanaume. Tena akutane na mtu anayejua kutongoza amuambie “Hivi na wewe kwanini unahangaika na lile lijamaa lako, mtoto mzuri kama wewe unakaa na mtu wa kulialia kama yule, uanjua unaishalilisha, mtu kila saa kanuna aiseee…” Nishamaliza, hata kama una wivu acha kumuonyesha, unaweza kumchunga mpenzi wako bila kuwa mtu wa kulalamika lalamika na kugombana kila saa.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA