ACHA KULAZIMISHA UPENDO KWA MCHUMBA WAKO AMBAE ANAONYESHA DALILI ZA KUTOKUTAKA TENA..

Inafika mahali lazima tukubaliane na ukweli,upo na mahusiano na mchumba wako ila anakuonyesha dalili fulani za ovyo,vitendo vya kujeruhi moyo wako,usiendelee kubembelezana na mtu wa hivyo utajipa matatizo mengine...ambayo hata ukuwa nayo.

Lazima tujue uchumba ni kivuli cha ndoa ikiwa mtu huyu ameanza kukuonyesha dalili za kukuchoka wewe ukafosi jua,hata ukiingia nae kwenye ndoa atakufanyia hayo na zaidi.

Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu,sasa kama umeona izo dalili kaa pembeni uwenda Mungu nae anakuonya mapema ndo maana ameweka tabia zake wazi.

Acha kuwa king'ang'anizi ukaingia kwenye ndoa na mtu wa namna hiyo,jua ni kujibebesha gunia la misumari.

Raha uchumba ni kupenda wote isiwe mwingine ni mtumwa wa mwanzake,,ikiwa unaona ni ngumu kukaa pembeni muombe Mungu akuwezeshe maana kwa nguvu zako ni ngumu .... 

Jiunge na group letu

https://chat.whatsapp.com/CVHMF6BPooMGeJhz01l8VI

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA