MAMBO 3 AMBAYO KILA MWANAMKE ANAPASWA KUYASAHAU ANAPOINGIA KWENYE MAHUSIANO MAPYA!


(1) Umri wako; Hata kama una miaka 40, lakini katika zile hatua za mwanzo wa mahusiano, miezi sita ya kwanza, acha kabisa kuwaza kuhusu umri wako, kuwaza kama unazeeka, kuwaza kama kwa uymti huo hutapata mtu wa kukuoa.

(2) Watu na Maisha yao; Kuna ndugu, kuna marafiki, kuna majirani na kila mtu anayekujua, wote wanataka uolewe, kuna kelele nyingi za kutaka uwe na mtotyo, uwe na mtu siriasi. Acha kuwawaza hao watu, furahia mahusiano yako na acha kuwaza wanakuonaje.

(3) Kuhusu kuwa na mtoto; Labda kama unaona kuwa kalenda yako inaelekea kufika mwisho, labda ushafikisha miaka 38 mpaka 40 ndiyo suala la mtoto linapaswa kukuumiza kichwa. Tofauti na hapo, unapoingia kwenye mahusiano jiondolee ile presha ya kwamba nitapata mtoto kweli, nisipozaa, mbona haonekani kama Baba na vitu kama hivyo.

Mambo haya matatu yanawasumbua sana wanawake. Wakiwaza kuhusu umri wkenda, nduguwa nanionaje na ile presha ya umti wangu unaenda bila mtoto wanakua na ptesha kubwa sana. kila wkaati unakua unawaza hivi akiniacha na umri huu nitaolewa na nani?

Watu watanionaje kuwa kila siku mimi ni mtu wa kubadilisha wanaume, unawaza hivi kweli kwa umri wangu si bora kuzaa tu, mbona haonekani kuwa siriasi, mimi nataka mtoto lakini yeye haeleweki. Kwa mawazo haya, hata mwanaume akifanya kosa kidogo, akibadilika kidogo basi unachanganyikiwa na kuona kama umeshaachwa.

Unakuta mwanaume mna miezi miwili, kaacha tu kukupigia siku mbili ila wewe ushapaniki, unaona kama unapotezewa muda wako, unawaza kuhusu kuachana ili angalau upate mwanaume mwingine ambaye wewe unaona kama yuko siriasi. Ukweli nikuwa wanaume wengi hawapendi kuharakishwa.

Wanataka mambo yajipe tu, mwanaume ajisikia raha na hamu ya kukuoa na si wewe kuulizia kila siku. Kama kila magusiano ndiyo kwanza yana miezi mitatu, ushaanza kupaniki, unamuona mwanaume kama kakuacha basi moja kwa moja unakua na kisirani na unamfanya akuchoke mapema.

Hivyo Punguza presha, ndoa kama ipo itakuja tu, kuitajataja sana sio kuikaribia. Lakini kama unaona unapresha sana hujui namna ya kufurahi, basi soma kitabuc hangu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” Bei yake ni shilling elfu kumi tu. Unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 

Hakikisha unapolipia jina linakuja Iddi Makengo kwanu kuna matapeli wengi na Kitabu unatumiwa kwa Whatsapp/Facebook/Email.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA