NI KITU KIDOGO LAKINI KINAFANYA NDOA YAKO IWE TAMU BALAA!


Hata kama umezoeana vipi na mume wako, jifunze kumuomba mume wako ruhusa na si kumpa taarifa. Haijalishi umemzidi kipato wala unatoka kwenye familia ya kitajiri kuliko yeye. Haka kautaratibu kanakupunguzia maudhi mengi sana, kuna mambo mengi utaepuka kama ukijijengea haka ka utaratibu.

Sio tu kama mume wako atahisi kuheshimiwa, lakini pia wewe itakufanya ujione mke. Mwanamke uhuru ukizidi sana anajiona mwanaume, anajiona kuwa anaweza kufanya chochote kile anachokiweza na kuna kashetani kanakuja kanakuambia umejaribu mume wako na hapo ndipo kila kitu kubadilika.

Narudia, najua mnahisi kuwa haki sawa, mbona yeye aage mimi niombe ruhusa, lakini ukweli nikuwa, mwanamke mume wako akiwa ni wa kukuomba ruhusa si tu utamchoka bali utajisikia kama umeoa. Mbali na kuwa ni heshima kumuomba ruhusa ila kuna kale kakudeka flani ambako wanawake wakikataliwa kitu wanakua nako.

Sio kwamba unapiga magoti au kuomba kama unaomba pumzi, lakini kama mmezoeana sana na mume wako hembu seba basi “Mume wangu kesho nilikua nataka nikitoka kazini niende kumcheki na Mama…” sio unafika kwa Mama ndiyo unamuambia “Niko kwa Mama nitachelewa kurudi hajisikii vizuri…”

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA