KAMA UNA TABIA HII KILA UNAPOINGIA ONLINE JUA UNAHARIBUA MAHUSIANO YAKO!


Kama ukiingia online, ukamuona mpenzi wako yuko online labda kwa nusu saa au masaa mawili bila kukutafuta unakasirika na kuhisi kuwa hakupendi, labda anachart na watu wengine, ukaona kama anakudharau basi jua kuwa una matatizo na unahitaji msaada, ni suala la muda tu utaharibu mahusiano yako.

Iko hivi, katika mahusiano ni lazima umpe fursa mwenza wako kukumiss, kufanya vitu vingine zaidi yako. Kama ukiingia kwenye mitandao, hamna kitu cha kuchart ushatuma meseji, ‘hi’ huna stori halafu unataka yeye ndiyo alete stori basi jua kuwa unakosea, ana haki ya kuwa online na ana haki ya kutokujibu meseji zako kama hajisikii.

Unapolazimishia kila dakika kuongea na wewe, kila dakika kuchart na wewe basi baada ya muda ataboroka. Hii ni kwa wote, wanawake na wanaume, yaani kama ni kuchart muwe na kitu cha kuchart, mwenzako naye apende na sio kwakua tu wewe huna kitu cha kufanya ulazimishie, na asipokua na mzuka wa kuchart unune, hiyo itakuharibia kila mahusiano.

NB; Kama wote mnapenda ndiyo starehe yenu basi hamna shida, ni raha sana kuchart na jibu meseji zake mfurahie, ila kama ukiona mwenzako hayuko kwenye mood, usinune, muelewe si kwakua hakupendi bali nikwakua ndiyo kawaida.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA