HII POST NI MAALUMU KWA VIJANA WA KIUME!

Hivi kwanini baadhi yenu mmekuwa washenzi na wapuuzi kiasi hiki??

Umemfuatilia binti wa watu kwa zaidi ya miezi sita.
Richa ya kukukataa na kukukwepa kwa kipindi chote hicho bado hukukata tamaa uliendelea kumfukuzia huku ukimuahidi furaha na mapenzi ya dhati

Kwa roho nyepesi kama tunavojua wanawake wameumbiwa roho ya huruma binti wa watu akaamua kukubali ombi lako si kwa kukupenda bali kwakukuonea huruma na kwa kujali muda unaopoteza kwaajili yake.

Ni kweli mwanzo hakukupenda lakini tangu alipokubali kuwa na ww taratibu akawa anakuweka moyoni mwisho wa siku akakupenda mazima.

Kutokana na ahadi zako ukamfanya aweke imani yake kubwa kwako akitegemea siku moja utakuja kuwa mume wake.

Sasa hata sijui uliitoa wapi hiyo roho ya kishetani
Baada ya kumfunua funua na kumchezea mtoto wa watu kwa zaidi ya mwaka na miezi ukaamua kumtelekeza na kwenda kuanzisha mahusiano na mwanamke mwingine.

Maskini binti wa watu kwa unyonge anakuuliza "Nimekukosea nini mpaka unifanyie hivo"
Kwa jeuri unajibu "eti hoo hujui kuoga, mara ww sio type yangu"

Hivi kwa kipindi chote cha miezi sita uliyokuwa ukimfuatilia
-Hukuona kama hajui kuoga??
-Hukujua kama sio type yako??

Umemvunja moyo binti wa watu kiasi cha kukosa imani na wanaume kwa ujumla
Akikaa anahisi wanaume wote duniani wako kama ww kitu ambacho si kweli.

Mtoto wa watu kageuka kuwa binti machozi kila siku analia kwaajili yako anajiuliza
-yako wapi mapenzi ya dhati uliyomuahidi kipini unampigia simu mara 8 kwa siku??
-haya machozi ndo furaha uliyomuahidi kipindi unamnunulia kifurushi hata kabla kingine hakijaisha??

Anakosa majibu anabaki kujuta kwanini alifahamiana na ww

Binti wa watu baada ya kukosa imani na wanaume kwa kipindi kirefu hatimaye kajitokeza kijana anayejali kamfungulia tena binti milango ya furaha na tabasamu kampendezesha na hatimaye katangaza ndoa

Sasa ww na upimbi wako kuona binti kapendeza unamfuata na kumpigia magoti eti unataka mrudiane.

"Really are you mad or something"
-------------------------------------------------------------------
Anyway:
Endelea tu na tabia yako ya kucheza na hisia za wanawake
Ila kaa ukijua laana ya usariti haitakaa ikuache mbali.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA