HUHITAKI KUJITAMBULISHA KILA SIKU KUWA WEWE NDIYO MWANAUME, WANAJUA!

Hakuna uanaume wowote katika kumpiga mke wako, hakuna kumfundisha kokote katika kumpiga. Uwezo wako wa kiakili ni mdogo kama unashindwa kukaa na mtu mzima ukaongea naye na mkaelewana. Haikufanyi kuwa na nguvu zaidi kama kila siku unampiga mke wako ambaye anakuheshimu na kukunyenyekea wakati ukifika ofisini unavumilia matusi na manyanyaso ya Bosi wako ambaye hata hana sababu ya kukutukana.

Acha kujishaua kua una hasira za karibu kwa mkeo anaongea sana hivyo huwezi kujizuia, hapanab ni kitu ambacho unaamua kwakua unamuona ni mnyonge, kwakua hujiamini vyakutosha hivyo unadhani kuwa labda ukimpiga ndiyo atajua kuwa wewe ni mwanaume. Kama wewe kila siku ni kumuambia mkeo kuwa “Utanijua mimi ndiyo nani humu ndani?” Basi jua hata wewe hujijui ni nani?

Simba dume hahitaji hata kunguruma ili kutambulika yeye ndiyo nani? Anajua kabisa yeye ni nani hivyo hahitaji kujitambulisha kila siku. Kama wewe ni mtu wa kujitambulisha kila siku basi jua kuwa kuna kasoro. Kama wewe unahitaji kumpiga mkeo ili ujisikie mwanaume basi jua kuwa una kasoro. Hemu baidilika jifunze kuongea na mkeo kama binadamu, kama unaongea na mtu mzima mwenzako halafu utaona kama hutakua na furaha.

Acha kujinunisha kila siku, kurudi nyumbani na mihasira ya ajabu ajabu, unawatishia watoto na kikubwa zaidi wakati ukidhani labda unamkomoa mke wako, ukidhani labda kwa wewe kununa anakuogopa na kukuheshimu hapana. Ameshakuzoea, ashazoe aujinga wako mpaka sasa anakuchukulia poa, hajali tena hivyo unaponuna na kudhani unamkosesha raha ni kama unajidanganya kwani yeye ashakuzoea na hajali hata ukiota miba usoni!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA